Google PlusRSS FeedEmail

CHRIS BROWN AKANUSHA KUVUTA BANGI

Mmoja wa wafanyakazi alisikikika akisema, “Nilimsikia Chris akisema nimelipia hii ndege dola 60,000 Kwa hiyo ninaimiliki kila kitu na hawa watu humu ndani ni wangu, huku akitoa moshi wa bangi aliyokua akiivuta”.

Kufuatia maneno hayo na habari kuendelea kusambaa kwamba Mkali wa R&B nchini marekani, Chriss Brown amevuta bangi ndani ya ndege na kupulizia moshi wa bangi kioo cha ndege , Jet aliyoikodisha kwa ajili ya safari ya utalii na kundi la vijana wenzake, ameibuka na kukanusha kwamba hakuwahi kufanya kitendo hicho.

Chris alionekana kuchukizwa na habari mbaya zinazotokea na kusambazwa kila kukicha kitendo ambacho amedai kinamfanya ajichukie hata yeye mwenyewe.
“Kuna muda mwingine naenda kwenye kioo kujiangalia, na najikuta naichukia taswira ninayoiona kwenye kioo”, alisema Chris Brown a/k/a Baba Royalty.

Mmoja wa vijana wenzake alisema, “Hakuna kitu kama hicho, hizo ni stori za uzushi kabisa. Chriss alivuta sigara nje ya ndege kabla ya safari na hakuvuta bangi akiwa ndani ya ndege”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging