Google PlusRSS FeedEmail

JENNIFER LOPEZ AMPONZA WAZIRI

Tamasha la Nyota wa Pop Jennifer Lopez nchini Morocco, limepelekea kutolewa wito wa kutaka waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo ajiuzulu.

Mjumbe mashuhuri wa Chama Tawala cha Haki na Maendeleo, amesema shoo ya mwanamuziki huyo katika tamasha la Mawazine Jijini Rabat, ilivunja maadili ya umma.

Waziri wa Mawasiliano Mustapha Khalfi, alikosolewa kwa kuruhusu tamasha hilo kurushwa kwenye kituo cha televesheni cha umma. Hata hivyo amegoma kujiuzulu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging