Google PlusRSS FeedEmail

LUDACRISE NA MKEWE WAPATA MTOTOJANA Mke wa Ludacris, Mwanamama Eudoxie alipost picha kwenye akaunt yake instagrama iliyoonyesha balloon (Puto) la mtoto nje ya nyumba yao liliandikwa baby Girl ikiwa na caption ya maneneno “She is here #blessed #grateful.”

Na baada ya muda kupita, Ludacris kwa kutumia instagram yake, alimpongeza mke wake kwa kumzalia mtoto wa kike.

Huyo atakua ni mtoto wa kwanza kwa Eudoxie, na wa tatu kwa Luda ambapo wawili wa mwanzo nao pia wakiwa ni jinsia ya kike aliwapata kwenye uhusiano wake uliopita.

Mtoto wao mpya wanamuita Cadence Gaƫlle Bridges, na dada zake ni Cai mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 6 huku mwingine anaitwa 18 Karma mwenye umri wa miaka 13.

Luda na Eudoxie walifunga ndoa mwaka jana na tangu wafunge ndoa mahusiano yao hayakuwa na kashfa na inaaminika hata habari hii ya wao kupata mtoto inaweza kuwashangaza wengi kwani hawakua wanafahamu kama Eudoxie anaujauzito.

Chanzo: www.power1051fm.com

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging