Google PlusRSS FeedEmail

WEMA SEPETU"NILIHAMASISHA WATU WAMPIGIE KURA ALI KIBA" , MAJINA YA WASHINDI WA TUZO ZA KTMA 2015
ULE Ushindani uliokuwa unaendelea katika mitandao ya kijamii huku mashabiki wa team hizi mbili za wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum, na Ali Kiba kuonekana kutambiana hatimaye jana utata umekwisha mara baada ya Ali Kiba kujizolea tuzo 6 za KTMA.

Huku Diamond Pltanum kujinyakulia tuzo 2, hali iliyoibua manung'uniko mbalimbali kwa baadhi ya mashabiki wa msanii huyo, ingawa ushindi wa Ali Kiba haujaweza kuvunja rekodi ya msanii huyo wa muziki ambaye mwaka jana alinyakua tuzo 7.

Baada ya ushindi huo, Pro-24 ilifanikiwa kuzungumza na msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, ambaye alionekana kumsaporty sana msanii wa muziki Kiba kwenye suala zima la tuzo naye alisema haya yafuatayo.

"Niliamua kuweka nguvu nyingi kwa kuhamasisha watu wampigie kura Ali Kiba kuweza kufanikisha ushindi wake ni kwa sababu, aliniomba kufanya hivyo kwa hiyo hata Diamond angeniomba pia ningefanya hivyo kiroho safi" alisema Wema.

MAJINA YA WASHINDI WA TUZO ZA KTMA 2015

1. KIKUNDI BORA CHA MWAKA – BONGO FLEVA – YAMOTO BAND

2. KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB – JAHAZI MODERN TAARAB

3. BENDI BORA YA MWAKA – FM ACADEMIA

4. MSANII BORA CHIPUKIZI – BARAKA DA PRINCE

5. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA (WAITE) -MRISHO MPOTO FT. FELLY KANO

6. WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA – NITAMPATA WAPI – DIAMOND PLATINUMZ

7. WIMBO BORA WA AFRO POP – MWANA ALI KIBA

8. VIDEO BORA YA MWANAMUZIKI YA MWAKA – MDOGOMDOGO – DIAMOND PLATINUMZ

9. MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA BENDI – ENRICO

10. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA BONGO FLEVA – NAHREEL

11. MTUNZI BORA WA MWAKA- HIP HOP – JOH MAKINI

12. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI – JOSE MARA

13. MTUNZI BORA WA MWAKA BONGO FLEVA – ALI KIBA

14. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB- MZEE YUSSUF

15. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIUME – ALI KIBA

16. MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIKE – VENESSA MDEE

17. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB – MZEE YUSSUF

18. MWIMBAJI BORA WA KIUME BONGO FLEVA – ALI KIBA

19. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB – ISHA MASHAUZI

20. MWIMBAJI BORA WA KIKE BONGO FLEVA – VANESSA MDEE

21. WIMBO BORA WA TAARAB (MAPENZI HAYANA DHAMANA)- ISHA MASHAUZI

22. WIMBO BORA WA MWAKA (MWANA)- ALI KIBA

23. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI (WALEWALE) -VIJANA WA NGWASUMA

24. WIMBO BORA WA R&B (SIKSIKII)- JUX

25. RAPA BORA WA HIP HOP – KIPI SIJASIKIA ( PROF J FT. DIAMOND PLATINUMZ)

26. MSANII BORA WA HIP HOP – JOH MAKINI

27. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI (SURA YAKO) – SAUTI SOL.

ENDELEA kusoma Pro-24 kwa habari mbalimbali za yaliyojili katika tuzo za KTMA.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging