Google PlusRSS FeedEmail

EX – BOYFRIEND WA NICKI MINAJ NAYE AMCHANA MEEK MILL

Lile beef linaloendelea kuwa gumzo mitandaoni baina ya marapa wawili kutoka nchini Marekani Meek Mill na Drake linaelekea kuchukua sura nyingine baada ya aliyewahi kuwa Boyfriend wa Nicki Minaj Safaree kuingilia kati na kumdiss Meek Mill.

Meek Mill ambaye kwa sasa ndiye Boyfriend wa Nicki Minaj siku kadhaa zilizopita alitoa maneno ya kejeli kwa kumuita Safaree kwamba sio mwanaume rijali

Meek Mill atoa maneno hayo huku akisisitiza kwamba Safaree sio mwanaume rijali sababu hakuwa anamridhisha Nicki walipokuwa kwenye mahusiano yao.

Safaree ameonyesha kukerwa na maneno hayo, hivyo aliamua kwenda studio na kurekodi track ambayo ni diss kwa Meek Mill.

Track hiyo tayari imeshaachiwa youtube na imepewa jina la Lifeline ina mashairi makali yenye lugha ya maudhi na moja kwa moja inamuongelea Meek Mill, kwamba ni rapa mdogo asiyelingana na Drake, hajui mapenzi na anaigiza maisha asiyoyaweza kuyaishi.

Beef baina ya Drake na Meek Mill lilianza wiki mbili zilizopita ambapo Meek alianza kwa kumshtumu Drake kwamba hajui kuandika mashairi na nyimbo zake nyingi huwa anaandikiwa.

Bofya Hapa Kusikiliza Track ya Safaree ambayo ni Diss kwa Meek Mill

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging