Google PlusRSS FeedEmail

KUKATWA KWA WEMA SEPETU BABA HAJI KICHEKO



STAA wa filamu Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ juzikati aliangusha sebene la nguvu kwenye Viwanja vya Ngome Kongwe, Zanzibar baada ya kupata taarifa kuwa staa wa kike nchini aliyekuwa akiwania nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu ameangushwa.

Akionekana mwenye furaha huku akiserebuka muziki alisema kuwa mbunge wenu amekosa ubunge, jambo lililowafanya baadhi ya wasanii wenzake waangue kicheko kwa kuwa inafahamika kuwa ana bifu naye.

“Jamani mmesikia majibu? Mbunge wenu kashika nafasi ya mwisho, ngoja mimi niendelee kucheza sebene langu,” alisikika Baba Haji huku akiangua kicheko.

Bifu la Baba Haji na Wema lilianza kitambo ambapo wawili hao walikutana kwenye Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar ambapo Wema alimchana jamaa huyo kuwa ananuka jasho.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging