Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WANAJIACHIA SANA- MONALISA

                     Yvpnne Cherryl
YVONNE Cherryl ‘Monalisa’ mwigizaji wa kike katika tasnia ya filamu Nchini amefunguka kwa kuwaambia baadhi ya wasanii katika fani ya uigizaji kushindwa kulinda miili yao na kujiachia kwa kunenepa na kupoteza muonekano wao jambo ambalo linapoteza nafasi zao katika sinema.

“Sisi wasanii wa filamu kwa Bongo hatuwezi kabisa kulinda muonekano wetu kimaumbo msanii akikubalika tu anajiachia mwili huo, vijana wadogo tu kuna wakati unashindwa umchezeshe kama binti au mama mtu mzima, lakini ukimuona msanii kama Sarafina yupo vile vile,”anasema Monalisa.

Monalisa anasema kuwa moja kati ya vitu muhimu katika tasnia ya filamu ni kuwa na mpangilio wa vyakula kufanya mazoezi ili kuendelea kuwa katika muonekano mzuri kama vile akina Angelina Jolie walivyodumu na hata badhi ya wasanii wengine Afrika ambao hawajapoteza mvuto kwa kujiachia kunenepa bila mpangilio.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging