Google PlusRSS FeedEmail

LUPITA NA NYWELE ZAKE



Muigizaji nyota mshindi wa tuzo la Oscar kutoka Kenya bi Lupita Nyon'go amesema kuwa anajivunia kuwa mwanamke mwenye nywele asili.

Lupita alisema kuwa licha ya kushamiri katika kilele cha anga za sanaa huko Holywood Lupita anasema anajivunia nywele zake asili.Lupita alipotua Hollywood

Lupita ambaye hunyoa nywele zake na wala hatumii dawa na kemikali za kunyosha nywele hizo anasema ''kama mwanamke mwafrika hana sababu ya kuaibikia muonekano wake asili''

''Nilihisi kama mtu aliyefunguliwa baada ya kukata nywele zangu zilizokuwa na kemikali ama ''perm''

Bi Nyong'o aligonga vichwa vya habari aliposhinda tuzo la Oscar kufuatia mchango wake katika filamu ya ''12 years a Slave''.Lupita alivuma katika filamu ya ''12 years a Slave''

kwa sasa anaigiza katika filamu ya ''Americanah'' ambayo iliandikwa na msanii Chimamanda Ngozi Adichie kutoka Nigeria.

lupita ametajwa kuwa balozi wa mazingira wa WildAid Wildlife

Kwa sasa bi Nyon'go aliyeteuliwa kuwa balozi wa maswala Mazingira wa shirika lisilokuwa la serikali la WildAid wildlife yuko nchini Kenya kuhamasisha umma kuhusu kazi hiyo yake mpya.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging