Google PlusRSS FeedEmail

MWANAMITINDO ABUNI VAZI LA SUTI KWA KUTUMIA ZIPU

Mwanamitindo na mbunifu wa mavazi nchini anayetambulika kwa jina la Dida Katona amebuni vazi jipya aina ya suti ya zipu.

Dida amesema kwamba anataka kuhakikisha taaluma na sanaa yake inafika mbali na kuipaisha nchi ya Tanzania tasnia ya sanaa ya mitindo na ubunifu huku akiielezea kwamba suti hiyo itakuwa ni ya kipekee.

Dida amesema, kwa mara ya kwanza vazi hilo liazinduliwa tarehe 8 Augost mwaka huu ndani ya ukumbi wa hoteli ya Regency Park iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.

Dida pia amewaomba watanzania kuthamini bidhaa zinazobuniwa na wanamitindo kutoka nchini Tanzania, kwani kufanya hivyo itawasaidia wanamitindo na wabunifu wengi kupata nguvu ya kuendelea kupambana kuhakikisha wanalitangaza taifa la Tanzania na sanaa ya mitindo na urembo kwa nchi nyingine duniani.

Dida, ni mwanamitindo na mbunifu wa mavazi ambaye mpaka sasa ameshafanya kazi na watu maarufu nnje na ndani ya nchi wakiwemo wasanii, Banana, Mrisho Mpoto, Mzee Yusuphu, Sarah na Muongozaji wa Video nchini Adam Juma.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging