Google PlusRSS FeedEmail

WASANII KURA ZA MAONI: WEMA SEPETU, KYSHER, PROF JAY WAPETA

Weekend hii kulikuwa kuna heka heka ya uchaguzi wa kura za maoni ndani ya vyama mbalimbali, ili kuwezesha kupatikana kwa wawakilishi wao katika ngazi mbalimbali uchaguzi mkuu 2015.

Mwaka huu tumeona pia muamko mkubwa kwa wasanii, na wadau kadhaa kujitosa kwenye medani za siasa.

Taarifa ikufikie kuwa tayari wasanii kadhaa wameshajua hatma yao weekend hii, katika upande wa wasanii Wema Sepetu, Khadija “Kysher” Shaaban, Wastara Juma waliokuwa wakiwania kuwakilisha mikoa mbalimbali Ubunge viti maalum CCM, ni Kysher pekee aliyefanikiwa kusonga mbele huku wengine wakishindwa kutamba.

Kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ Mikumi, mshindi na mmiliki wa tuzo ya wimbo bora wa Hip Hop KTMA2015 Joseph ‘prof jay’ Haule, anatajwa kuibuka kidedea katika kura hizo za maoni kutoka CHADEMA jimboni humo.

Tazama ‘post’ walizoandika Wema Sepetu, Wastara na Kysher baada ya matokeo kutangazwa.

“Nilivyo amua kugombea viti maalum, nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa, ila dunia bado inazunguka. Nawapongeza walioshinda. Nawashukuru mlioniunga mkono, Mungu aendelee kuwabariki kwa mapenzi yenu juu yangu, yananipa moyo.

Nawashukuru pia wote mlionipinga maana mmeniongezea ujasiri na nina nguvu mpya ya kuthubutu upya. 2015 ni mwaka wa kipekee kwenye muamko wa vijana Tanzania. Bigger things loading.. Most of all Nilizaliwa nikiwa katika Chama Cha Mapinduzi na nitakufa nikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi…. Safari yangu ya Siasa ndo kwanza inaanza…” ameandika Wema

“‘mara nyingi watu wanakosa uthubutu kutokana na kutojiamini kuwa vile walivyo wanaweza kufanya mambo makubwa ya ajabu bila kujali kiwango cha elimu, pesa au mtandao alionao” haya ameyaandika Kysher.

“Morogoro tumebarikiwa ukarimu mmenibeba mmepokea mmenikumbatia na mwisho mmenililia kwa mapenzi yenu makubwa mlionyesha kwangu siwaachi ng’o na walemavu wa nchi nzima waliokuwa bega kwa bega wakilia na mim na kuniombea mafanikio sijashindwa bado sababu nina nia ya kweli juu yenu juu yetu kuhakikisha tunaheshimika na shida zetu zinatatulika nitatumia fursa niliyonayo kuwafikia,” Wastara.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging