Google PlusRSS FeedEmail

BATULI AMPA ONYO KALI KITALE

MSANII wa filamu nchini hatimaye amefunguka ya moyoni mara baada ya picha zake zikimuonesha yupo katika mahaba mazito na msanii mwenzake Stan bakora  kusambaa kwenye mitandao, huku baadhi ya watu wakidai kuwa wanamahusiano.

Msanii huyo ameshangazwa na kitendo hicho cha kuzagaa kwa picha hizo na kudai kuwa hizo picha ni miongoni mwa vipande vilivyopo kwenye movi yao mpya aliyocheza na msanii huyo katika kipande cha mapenzi.

"Kwanza mniwie radhi watanzania mnachokiona na kinachoendelea ni vitu viwili tofauti mwenye akili timamu anapata jibu kamili @mkudesimbaoriginal nakuuliza hivi wakati unamapa @matejamusa picha ulimwambia ni za nini? hivi naweza kuwa faragha mbele ya camera? hata kama unapromote movie hii sio kiivyo kama kupromote kitu ndio hivi basi fani yetu imejaa mazumbukuku, hii scene iliyopo kwenye movie sioni sababu ya kunichafua kijinga hivi, kizuri kinajiuza" aliandika Batuli kwenye ukurasa wake wa istagram.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging