Google PlusRSS FeedEmail

SAID FELLA APETA KURA YA MAONI UDIWANI KATA YA KILUNGURE

Wadau wawili wa michezo na burudani nchini; Yusuf Manji na Said Fella wameibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha udiwani katika jimbo jipya la Mbagala jijini hapa.

Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group, alishinda katika udiwani katika Kata ya Mbagala Kuu wakati Fella ambaye ni msimamizi wa kazi za wasanii na muasisi wa Kundi la Mkubwa na Wanawe, alishinda katika Kata ya Kilungure.

Fella ni Meneja wa mwanamuziki maarufu nchini, Diamond Platnumz, TMK Family na Yamoto Band. Kaimu Katibu CCM Wilaya ya Temeke, Rutami Masunu alisema uchaguzi huo ulikwenda vizuri katika maeneo mengi isipokuwa changamoto kidogo katika kata moja ambayo itafanya uchaguzi huo leo.

Alisema tayari matokeo ya kata 28 kati ya 32 za wilaya yake yamewasilishwa ofisini kwake na baada ya kuyapitia na kukusanya taarifa zinazowahusu madiwani na wabunge na muda wowote leo atatoa taarifa kamili.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging