Google PlusRSS FeedEmail

CHILAMBO HAJAWAHI KUTUMIA HELA YA BSSMshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba Bongo Star Search wa mwaka 2012 Walter Chilambo amesema mpaka sasa hajawahi kutumia mkwanja aliowahi kuupata kwenye Shindano hilo kwa shughuli zake za muziki.

“Pengine BSS inafaida zaidi ya ule mkwanja anaoupata mshindi, Milioni 50 nilizozipata nimezitumia kwa mambo mengine kabisa kama kununua gari na mengine ya kimaisha zaidi ya muziki” Walter Chilambo alifunguka hayo.

Chilambo amesema, kazi zake za muziki nyingi alikuwa anasimamiwa na kampuni ya simu ya zantel, na wadau wengine wa muziki kwani uwezo wake na Baraka alizozipata toka BSS zilifanya nyota yake ing’are na kuaminika kwa kila mdau wa muziki.

“Kuna kipindi naenda studio, unakuta Producer ananizawadia beat, nami kwa kuwa ninaifanyia kazi nzuri basi sikatwi hela yoyote”, alisema Walter Chilambo.

Chilambo pia ameishukuru BSS kwani imemfungulia njia ya maisha yake ya kimuziki huku akiwataka wasanii wanaoshiriki BSS kwa sasa wazingatie wanachojifunza ndani ya shindano hilo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging