Google PlusRSS FeedEmail

SIR ELTON JOHN ATAMANI KUKUTANA NA VLADIMIR PUTIN

                           Sir Elton John amesema angependa sana kukutana na Vladimir Putin wajadiliane kuhusu alichosema ni mtazamo wa kushangaza wa kiongozi huyo wa Urusi kuhusu haki za mashoga.

Ripoti ya shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch mwaka uliopita iliishutumu Urusi kwa kushindwa kuzuia mashambulio dhidi ya watu wa makundi yanayobaguliwa na kutochukulia hatua wanaotekeleza mashambulio hao.

Sir Elton amesema angefurahia sana kukutana na Putin ingawa anajua kwamba baadaye huenda kiongozi huyo akamcheka na hata kumuita mpumbavu.

Mwanamuziki huyo kwa sasa yuko Ukraine ambako alihimiza kuwepo kwa haki zaidi kwa mabasha na wasagaji.Urusi, ambayo ni jirani wa Ukraine, Juni 2013 ilipitisha sheria iliyolenga kuadhibu watu binafsi wanaoendeleza “tabia za ushoga miongoni mwa watoto”.

Sir Elton alishutumu hatua hiyo, pamoja na matamshi ya Bw Putin aliyoyatoa mwaka jana, akiashiria kuwa mashoga waliwaandama watoto.

“Wewe ni Rais wa Urusi, na unasema jambo la kipuzi kama hilo?”

Alisema mtazamo wa Putin kuhusu mashoga ni wa “kuwatenga na kuwabagua” na wa “kushangaza”.

"Ningependa kukutana na [Bw Putin]," Sir Elton aliambia waandishi wa habari

"Huenda akanicheka baadaye, na kuniita mpumbavu, lakini angalau nitakuwa nikijua kwenye dhamiri yangu kwamba nilijaribu.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging