Google PlusRSS FeedEmail

FRANK AJIPANGA KUWATUMIKIA WAKAZI WA SEGEREA

MSANII wa filamu nchini ambaye alikuwa mgombea wa Ubunge katika jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, kupitia chama cha ACT-Wazelendo Frank, amedai kuwa anadeni la kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

Mwigizaji huyo Frank alijitokeza kugombea Ubunge jimbo la Tabata Segerea kupitia tiketi ya ACT-Wazalendo lakini kutokana na kura zake kuwa chache hakufanikiwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.

Alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo walimpokea vizuri na kumpa ushirikiano katika kipindi chote cha kampeni, aliongezea kuwa mbali na kushindwa anampongeza na atashirikiana na mshindi wa jimbo hilo.

Alisema kuwa mbali na kushindwa anajipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao, huku akibainisha kuwa uchaguzi ulijawa na changamoto nyingi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging