Google PlusRSS FeedEmail

PROF.JAY KUTEKELEZA ALICHOKIAHIDI MIKUMI

BAADA ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Prof. Jay kutangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la Mikumi, Morogoro zimeibuka habari mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii na kudai kuwa huyu ni mbunge wa wananchi wa Mikumi na si mbunge wa Wasanii.

Hali hizo zilienea kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wake wakimpongeza kwa kuweza kufanikiwa kutwaa ubunge huo, ambapo wapo waliotoa pongezi na wengine kudai kuwa si mbunge wa wasanii ni mbunge wa wanamikumi.

Prof. Jay amesema amefurahia ushindi huo, huku akiahidi kutekeleza Ilani ya chama chao ili kufanikiwa kupeleka maendeleo katika jimbo lake.

Amedai kuwa maendeleo kwenye jimbo hilo ni ya kila mtu bila ya kujali itikadi. Huyu ni msanii wa pili wenye majina kwenye tasnia ya muziki walioamua kujiingiza kwenye siasa na kuweza kufanikiwa kushinda Ubunge.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging