Google PlusRSS FeedEmail

JACQUELINE WOLPER : LOWASSA KIONGOZI SHUPAVU


MSANII wa filamu nchini  Jacqueline Wolper Masawe, amesema kwake yeye aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA Edward Lowassa ni kiongozi shupavu na jasiri.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wolper amemwagia sifa lukuki waziri mkuu huyo wa zamani na kuwataka Watanzania kuwa pamoja katika kuijenga nchi.

“Ndugu zangu Watanzania kwanza nitoe shukrani za dhati kwa kwa viongozi wa UKAWA katika kipindi chote cha kampeni,Napia natoa pongezi za kipekee kwa Mh Edward Ngoyai Lowassa kwa kuweza kuwa shujaa kupambana kwa kutuletea mabadiliko Watanzania kwasababu ameweza na ametuonyesha mapambano km anaweza kwa kutoka CCM kuja UKAWA,

Na pia naamini umeleta historia kubwa sana hapa nchini kwasababu haijawahi kutokea hapa TZ,Hatujafanikiwa kwenda Ikulu lakini naamini Mh Lowassa ametuma ujumbe kwa viongozi wengine ambao walikua wazembe na waliojisahau na wataifanya TZ iwe mpya kupitia mabadiliko alioleta Lowassa,Pia naamini yalitokea mambo mengi kipindi cha kampeni tumekoseana kisiasa na wasanii wenzangu ili tu kuiweka nchi yetu Imara,

Mimi Jackline Wolper napenda kuwashukuru wotee tuliokuwa pamoja kwenye maswala ya uchaguzi kuanzia wasanii mpk mashabiki zetu.Pongezi pia kwa Magufuli kwa kuweza kushinda cha msingi asisahau ahadi alizowaahidi wananchi kipindi cha kampeni,wananchi wanataka mabadiliko..Mimi bado ninaamini Lowassa ni kiongozi shupavu,muelewa na mwenye akili za kupambanua mambo kushindwa kwake haijalishi kwa sababu naamini watz wanamkubali hasa kwenye mabadiliko,kwa wasanii wenzangu ambao mpo CCM tusijengeane chuki kwa yaliyotokea kwani niliamua kutafuta haki yangu ya msingi nikiwa km msanii,

Kwa wana mabadiliko wenzangu tuendelee kupambana mtakao tuwakilisha bungeni mfanye kazi ya maana hasa kuwatetea wanyonge msijisahau…Mungu Ibariki Tanzania peoples power!” ameandika Wolper.

Edward Lowassa amepata asilimia 39 katika uchaguzi mkuu kiti cha Urais mwaka huu, akiachwa mbali na mpinzani wake wa karibu aliyeibuka kidede wa kiti hicho J.P Magufuli wa CCM kwa asilimia 58.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging