Google PlusRSS FeedEmail

CHARLIE SHEEN ASEMA ANAISHI NA VIRUSI VYA HIV


Muigizaji nguli wa Hollywood, Charlie Sheen amejitokeza wazi na kufichua kuwa anaishi na  virusi vya ukimwi.Sheen aliyepata umaarufu zaidi kwa kuigiza katika filamu ya ''Two and a half men'', alifichua hali yake katika mahojiano na runinga ya Marekani.

‘’Niko hapa kukiri mimi nina virusi’’ ‘’Ni maneno machungu’’ alisema.Sheen amesema hafahamu alikotoa ugonjwa huo ila analaumu unywaji wa pombe na madawa ya kulevya kwa hali yake.

Muigizaji huyo ameongeza kusema kuwa anaendelea kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi na amekuwa akifuata maagizo kwa umakini.Sheen alimsimulia mtangazaji wa NBC, Matt Lauer kuwa alichoshwa kuwalipa watu pesa iliwafiche hali yake kutokana na unyanyapaa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging