Google PlusRSS FeedEmail

CJAMOKER AELEZA SABABU ZA KUFANYA KAZI NA MABESTE"Hold on" ni moja kati ya ngoma zake kali ambazo zimezidi kumuweka pazuri katika ramani ya muziki wa bongo fleva.Cjamoker ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki licha ya kuwa rapper na muimbaji wa muziki wa bongo fleva.

Sijaona ni wimbo wake unatarajiwa kutoa hivi karibuni ambapo amemshirikisha msanii Mabeste.

Akizungumzia sababu zilizompelekea kuamua kufanya kazi na Mabeste Cjamoker alisema kuwa msanii huyo uwezo wake wa kufanya ngoma kali ndio unaochangia kuamua kufanya naye nyimbo mara kwa mara.

”Naachia tena ngoma mpya kutoka kwangu, kama ilivyokawaida yangu nimeaandaa kila kitu mwenyewe kuanzia mdundo hadi kurecod, na hii ngoma nimefanya na Mabeste, licha ya watu wengi kusema kwanini nafanya ngoma mara nyingi na jamaa lakini ni kwamba Mabeste ni rapper mkali na sio vibaya kufanya kazi na mtu mara kadhaa kwaiyo uwezo wake ndo unafanya nitamani kufanya nae kazi kila iitwapo leo.

Wimbo wangu wa sijaona ni wimbo wa mapenzi ambao unahusisha sifa za mwanamke ambaye kutokana na mazuri mengi aliyokuwa nayo nimezungumza nimekuwa na mademu lakini sijawahi ona kama yeye.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging