Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND NA VANESSA MDEE WANYAKUA TUZO ZA AFRIMA

Wakali wawili wa muziki wa Bongo Flava, mwanadada Vanessa Mdee na ‘Icon’ wa Africa Diamond Plutnumz wako nchini Nigeria kwa shughuli za kimuziki.

Mbali na kufanya ‘media tour’, walihudhuria pia hafla ya utoaji tuzo za ‘All Africa music awards’ (AFRIMA) zilizotolewa jana usiku mjini Lagos.

Diamond aliyekuwa akiwania ‘tuzo’ hizo, amefanikiwa ‘kuzivuta’ 3 nyumbani Ikiwemo ile ya msanii Bora wa mwaka iliyokuwa ikiwaniwa na Ali Kiba, Davido, Sarkodie, Wizkid, Yemi Alade, Jose Chameleone na Flavour.

Nyingine ‘aliyoibugia’ ni ya msanii bora wa Afrika Mashariki pamoja na wimbo bora wa mwaka.

Vanessa yeye alifanikiwa kuinyakua tuzo ya wimbo Bora wa Afro Pop.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging