Google PlusRSS FeedEmail

IDRISS SULTAN ASHIKWA KIGUNG'UMIZI MAHUSIANO YAKE NA WEMA SEPETU

Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014 na ‘mchekeshaji’ kiwango Bongo Idriss Sultan, amesema kwa sasa malengo yake ni kuukwaa Ubilionea.

Akizungumza kupitia kipindi cha ‘The playlist’ cha Times Fm, Idriss amesema mwanzoni ndoto yake ilikuwa ni kuwa ‘milionea’, kitu ambacho amekikamilisha kwa sasa kupitia BBA na anachokiangalia ni kutoka hapo alipo na kuvuna ‘mkwanja’ mrefu zaidi.

” Unajua mi ni mtu siku zote wa kutaka kupiga hatua, mwanzoni nikasema nataka kuwa milionea, lakini sasa hivi pia nataka nielekee kwenye Ubilionea.

Sasa kama mtu bado huna nyumba ya pili ya kutegemea, na bado huna ‘private jet’ wala nini, bado huna gari kali inabidi nizitafute tu ili mwisho wa siku nipaki gari kali pembeni ya ndege yangu mwenyewe” alisema.

Katika ‘line’ nyingine, mkali huyo alishindwa kufunguka ‘kinagaubaga’ mahusiano yake na Actress Wema Sepetu licha ya kuonekana na gari la malkia huyo wa filamu Bongo mara kwa mara.

Idriss pia alifunguka ‘exclusive’ kuwa, show yake ya TV itaruka kupitia kituo cha Luninga cha kimataifa cha BET.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging