Google PlusRSS FeedEmail

DULLY ASHANGAZWA NA WASANII WASIOPENDA KUANDIKIWA NYIMBO

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Dully Sykes 'Mr Misifa' ameweka wazi kuwa wimbo aliouachia juzi unaoitwa 'Tuache' ameandikiwa mashairi na kundi la muziki la Yamoto Band.

Ambapo amebainisha kuwa hiyo ni nyimbo yake ya pili kuandikiwa mashahiri ambapo nyimbo yake ya kwanza kuandikiwa ilikuwa wimbo wa Dhahabu na kijana aliyejulikana kwa jina la Jay C.

Dully ambaye ameachi kibao chake cha “tuache”alichofanya na Yamoto Band.Wimbo huo wa tuache ni wimbo ulioandikwa na vijana wa kundi la Yamoto Band.

Dully hakusita kueleza wazi juu ya kitendo cha kuandikiwa wimbo huo ambapo alisema”Watu hawajui tu huu sio wimbo wa kwanza mimi kuandikiwa ni wimbo wangu wa pili.Na kama msanii hutaki kuandikiwa ujue wewe sio manii maana hata Michael Jakson amewahi kuandikiwa.

"Dhahabu ni wimbo wangu wa kwanza kuandikiwa aliandikia Jay c zile versr zangu zote aliandika huyu jamaa.Kwahiyo huu wimbo wa tuache umeandikiwa na yamoto band me nilichofanya ni kutengeneza mdundo na kuingiza sauti basi.”alisema

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging