Google PlusRSS FeedEmail

DULLY SYKES: P FUNK MAJANI NDIO PRODUCER MSOMI NCHINIKing wa Bongo Flava Dully Sykes, amesema kwake yeye mtayarishaji wa muziki kitambo Bongo P Funk Majani ndiye namba moja Afrika Mashariki.

Akizungumza kupitia kipindi cha ‘The Jump Off’ cha Times Fm, Dully amedai hakuna anayekataa kwamba Majani ni msomi katika mambo ya muziki.

“Hakuna anayekataa mziki aliokuwa anaufanya Majani, ni amesomea unajua, sijui kati kuna nini mpaka haonekani.

Mi nakwambia ni Producer namba moja na Bora Afrika Mashariki, na hakuna anayekataa, hatuwezi tu kujua hapa kati kuna nini” alisema Dully.

Katika ‘line’ nyingine, Dully amedai kwa sasa hakuna mtayarishaji aliyesoma zaidi ya Hermy B, Dunga na Chizen Brain.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging