Google PlusRSS FeedEmail

FAIZA ALLY ATOA TANGAZO LA BIRTHDAY YA FAIDA

MSANII wa filamu nchini ambaye pia ni mzazi mwenzake mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Mh. Sugu, Faiza Ally ametoa tangazo kupitia ukurasa wake wa Istagram juu ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa inayotarajia kufanyika December 17 mwaka huu.

Faiza ni msichana ambaye amejipatia umaarufu mkubwa hasa katika vituko mbalimbali anavyokuwa anafanya.Moja ya kituko chake ilikuwa ni kuvaa pampers siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa.Licha ya hivyo nyingine ni ile ya kuvaa nguo iliyomuacha wazi eneo kubwa la mwili wake. Hali iliyosababisha ugomvi na mvutano mkubwa kwa mzazi mwenzake hatua zilizopelekea mbunge huyo kumfungulia mashtaka mahakamani.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliandika hivi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, “TANGAZOOOO December 17 ndio birthday yangu ntakua na miaka 32!!!!! nataka nifanye iwe yenye faida zaidi kwa watoto wanao hitaji- nitaweka kiingilio cha shilingi elfu 30 ntaanza kuuza hivi karibuni – na pesa hizo zitaenda kwa watoto yatima na watoto wanao hitaji misaada yetu….. Lkn pia tuta enjoy …. Tutakata keki – tutakunywa na kucheza mziki – tutapiga picha na kufahamiana zaidi…..kwa hivyo tuta enjoy na tutasaidia – pia nitaweka tiketi za VIP kwa sh elfu 50…. Na zitakua 20 tu! Nataka wewe umwambie mwenzio na mwenzio amwambie mwenzie- bila kusahau vivazi flan amazing.Tag rafiki yako na rafiki yako atag mwingine tuenjoy na huku tukitengeneza tabasamu kwa watoto wetu na pia kwa yoyote atakae kuwa anasheherekea birthday yake na mm atakuja na keki yake tufurahi pamoja – hapo vipi?”Ameandika

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging