Google PlusRSS FeedEmail

FID Q YUPO TAYARI KULIPA DENI

MSANII wa miondoko ya Hip Hop Fid Q, amesema kuwa yupo tayari kulipa deni la mashabiki wake wa muziki huo wanaomdai video mpya na nyimbo mpya huku akisisitiza kuwa dawa ya deni ni kulipa hakuna namna nyingine.

Msanii huyo ambaye ameonekana kukonga nyoyo za mashabiki wake katika jukwaa la Coke studio,ambapo ameshirikiana na msanii Maurice Kirya.

Fid Q ni miongoni mwa  wasanii ambao wamekuwa wapo karibu zaidi na mashabiki wake hasa katika mtandao wa Twitter.Fid q hakusita kumjibu mshabiki wake baada ya kumwambia”blaza tunahitaji mkono mpya maana kimya kimezidi.Fid Q hakusita kumjibu mshabaiki wake na kusema ” kumuuliza kuhusu ujio wake mpya,Ambapo Fid alisema”Nadaiwa video tatu nitazilipa soon”.

Fid Q aliwahi kusema kuhusu video zake tatu katika kituo kimoja cha radio wakati akifanya mahojiano,na mpaka sasa tayari imeshapita miezi kadhaa.HIvyo kama anakumbuka deni hilo mashabiki wake muendele kusubiri pia na kumdai maana ahadi ni deni.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging