Google PlusRSS FeedEmail

MAGUFULI WASHUKURU WASANII

                           

HAIKUWA kazi rahisi katika kuusaka urais kwa awamu ya tano kila chama kilitumia mbinu katika kuhakikisha kinaibuka kidedea, na hatimaye Dr. John J Pombe Magufuli kuteuliwa kuwa Rais wa awamu ya tano, Mh. Rais mteule amewashukru wasanii kwa support yao wakati wa kampeni

               Nasib Abdul, Amri Athuman
“Nawashukru sana wasanii kwa mchango wenu tulikuwa wote katika kampeni nimeona mchango wenu, kiukweli mmenibeba na nitahakikisha haki zenu zinalindwa na kuwa na mfuko wa wasanii ambao naamini utakuwa msaada kwenu”,anasema Dr. Magufuli.

                 Wema Sepetu, steven mengele, Yobnesh Yusuf
Ni nafasi nyingine kwa wasanii kuwa karibu na taasisi kubwa kama rais ni kuwa makini na kutengeneza umoja kukaa pamoja na kuweka vipaumbele muhimu katika tasnia ya filamu na muziki huku pia mkiungana pamoja na kuachana na itikadi za vyama kwani tunahitaji mawazo ya pamoja.
                 Simon Mwakifwamba
Naye Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon mwakifwamba amempongeza Mh. Dr. Magufuli kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwaka

“Hongera sana Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano tunakuombea afya njema,ufanisi na utendaji bora katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi,”

“Na ustawi wa watanzania na kwa sisi pia kujitoa na kukuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii kwa kila mmoja wetu kusimamia wajibu wake. Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania,”alisema Mwakifwamba.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging