Google PlusRSS FeedEmail

HARMONIZE AMPIGA CHENGA YOUNG THUG

Chipukizi wa muziki wa Bongo Flava aliye chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby(WCB) aitwae Harmonize, amesema ‘habadan’ hamkubali na hatokuja kumuelewa rapper wa Marekani Young Thug.

Akipiga ‘story’ kupitia kipindi cha Bongo.home cha Times Fm, Hit maker huyo wa Aiyola amedai matendo ya rapper huyo yamemfanya yeye kumuondoa miongoni mwa rappers anaowakubali.

“Thug ni kama kaokota Embe kwenye Mkwaju, ni bahati tu katoboa ashukuru sana, we angalia jinsi vitendo vyake vinavyotia shaka” alisema Harmonize.

Hivi karibuni rapper Young Thug, alifunguka kuwa anapenda sana kuvaa jinsi za kike kwa kuwa zinampendeza, kauli ambayo imeibua maneno miongoni mwa mashabiki wa muziki Duniani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging