Google PlusRSS FeedEmail

MISS TANZANIA KUCHUANA NA WAREMBO 100 MISS WORLDJOTO la kumtafuta mrembo wa dunia limepamba moto, ambapo baadhi ya warembo kutoka nchi mbalimbali wamewasili nchini China kwa ajili ya maandalizi ya shindano hilo huku kila mmoja akijinadi kunyakua taji hilo.

Miss Tanzania Lilian Deus ndiye mrembo anayepeperusha bendera ya Tanzania katika shindano hilo, ambapo ameshatua nchini humo kuungana na warembo wengine tayari kwa maandalizi ya fainali za Miss World 2015.

Miss Tanzania atachuana na warembo zaidi ya 100 kutoka nchi mbalimbali wanaoshiriki fainali hiyo ya mrembo wa Dunia, ambapo warembo hao wanatarajia kukaa kambini kwa muda usiopungua wiki nne.Lilian aliondoka Tanzania Novemba 19 mwaka huu.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging