Google PlusRSS FeedEmail

NAHREEL ASHANGAZWA NA WASICHANA WA SIKU HIZI

MTAYARISHAJI wa muziki wa kizazi kipya nchini Nahreel ashangazwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya akina dada kutaka mafanikio ya haraka kwa kutumia njia ambazo si harari, hali inayopelekea kushindwa kutimiza ndoto zao.

Aliyazungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Mkasi ambapo alisema kuwa wadada walio wengi siku hizi wanapenda zaidi mambo ya haraka haraka bila ya kujali ndoto zao, zamani wadada wengi walikuwa wanaishi na ndoto zao na kuzitimiza.

”Siku hizi nashangazwa na wadada walio wengi,unajua wadada wengi wa sasa hawana ndoto.Wanapenda zaidi mambo ya haraka haraka.Zamani wadada walikuwa na ndoto mfano zamani mtu anasema nataka niwe daktari au nataka kuwa fulani kitu ambacho hakipo sasa kwao.”

Nahreel pia alisema kwenye suala lake la studio anaweza akampa msanii beat na kama hajaifanyia vizuri akamnyanganya na kumpa msanii mwingine.si kwa lengo baya ila kama unashindwa kutendea haki mdundo ni wajibu wangu kumpa mwingine.”alisema

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging