Nicki Minaj kutoka Cash Money Records kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wa miaka 12, Safaree Samuels Miezi michache iliyopita Nicki Minaj na Safaree Samuels walishambuliana kwenye mitandao ya kijamii huku Safaree akidai Nicki alianza mahusiano na Meek Mill wakati bado wapo pamoja… Safaree amesema anaenda moja kwa mojaMahakamani kudai kilicho chake!
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Safaree amepeleka madai yake Mahakamani na kutaka asilimia yake ya pesa kutoka kwenye Album tatu za Nicki Minaj: The Pinkprint, Pink Friday na Pink Friday: Roman Reloaded, huku akidai pesa kubwa zaidi ya pesa kwenye mauzo yaliopatikana kwenye single 3 kubwa za Nicki, Only aliyomshirikisha Chris Brown, Drake na Lil Wayne, Flawless (Remix) wimbo aliofanya na Beyoncepamoja na share yake kwenye wimbo wa Feeling Myself aliomshirikisha Beyonce Knowles.