Mwalimu Rashid Masimbi akichangia kwa hisia kali juu ya Maadili katika Filamu zetu.Kulia kwake Ni Mkongwe wa Muziki wa Dansi,Kassimu Mapili
Wadau,kama kawaida leo hapa Baraza la Sanaala Taifa (BASATA) kwenye Jukwaa la Sanaa kulikuwa na Mjadala Mkali kuhusu Filamu za Kibongo na maadili yake kwa jamii za kitanzania.
Mjadala huo uliohudhuliwa na zaidi watu 100 na kuchokozwa na Rais wa Chama Cha Wamiliki wa Video Library,Richard Kallinga, ulijikita kwenye haja ya waandaaji wa filamu za kibongo kutengeneza filamu zenye ubora, zenye kubeba maadili ya mtanzania, zilizo na uhalisia wa maisha yetu ya kila siku,zisizokuwa za kuiga kutona Nollywood (Nigeria), zenye ujumbe unaoeleweka na kwa ujumla zenye mvuto.
Katika mjadala wake, wadau wengi walisema kwamba, Industry ya Filamu hapa Bongo imeajiri vijana wengi na inafanya vizuri ila hawakusita kutaja matatizo sugu ambayo lazima yafanyiwe kazi ili kubadili industry hii ambayo hapana shaka imekuwa kimbilio la wengi.Matatizo yaliyoainishwa ni pamoja na:
1. Wizi wa kazi za wasanii (Piracy) ambapo ilishauriwa kwamba Cosota lazima ibadilike, ipewe meno na iweze kupambana vilivyo na tatizo hili ambalo limekuwa likiwakwamisha wasanii wengi.
2. Kunakiri (copying) kazi za wasanii wa Nigeriana kutumia muziki (Sound Tracks) za wasanii wa muziki bila idhini yao.Katika haya wasanii wa Filamu wameshauriwa kuwa makini kwani sheria ya Hakimiliki inaweza kuwafunga.Kwa ujumla wasanii walishauriwa kuwekeza ubunifu binafsi na kubeba uhalisia wa sanaa yetu badala ya ilivyo sasa ambapo filamu zetu zimekuwa zikifanana fanana na zile za Nigeria.
3. Uchafu wa Filamu-Wadau wengi wamesema kwamba, filamu za kibongo zimekuwa na maadili mabovu yanayotokana uvaazi wa vichupi kwa wasanii wa kike, uoneshaji wa matendo ya faragha (mapenzi) mara kwa mara, script zenye kushabikia matendo maovu na yasiyofaa kwa jamii nk.Wadau walishauri Bodi ya Filamu, vituo vya TV na wasanii wenyewe kuhakikisha wanadhibiti filamu zisizo na maadili kwani zimekuwa zikitia aibu/kichefuchefu.Ilielezwa kwamba, baadhi ya filamu hazibebi uhusika wenye ufanano na maisha/maadili ya kitanzania
4. Wasanii kuact maisha ya juu mara kwa mara tofauti na uhalisia wao.Mtaalamu wa Filamu kutoka Chuo Kikuu,Bw.Ndunguru alieleza kwamba,filamu nzuri ni ile inayobeba uhalisia.Aliongeza kwamba, wasanii wanapenda kutumia magari ya gharama kama Hammer, majumba ya thamani, maisha ya anasa nk. kwenye filamu zao kueleza uhalisia usiokuwepo katika maisha yetu.
5.ubunifu mdogo wa waongozaji ,watengenezaji na mameneja wa filamu ambao wamekuwa wakifanya muda mwingi kunakili (copying)kazi za kigeni ,ilishauriwa kwamba ,wataalamu hawa wafikirie walau kupata elimu ,semina na mafunzo ya muda mfupi kwenye taaluma zao
6.kutozingatia mikataba kwenye kazi zao.ilielezwa kwamba ,wasanii wengi wamekuwa wakilalamikia wasambazaji wa kazi (Distributors)huku wakiwa wamesainiana mikataba,kumbe tatizo lililopo ni wasanii wenyewe kusain mikataba kwa pupa,ni uroho wa fedha ,bila kuisoma mikataba husika na wakati mwingine bila kuandikiana bali hufanyika mazungumzo ya mdomo tu.ilishauriwa wasanii wasimamie mikataba na kuhakikisha inawafikisha katika mafanikio.wasilalame tu,wachukue hatua pia