Google PlusRSS FeedEmail

H-BABA ACHIA FILAMU YAKE...


Mwanamuziki  mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleva Hamis Ramadhani Baba (H. Baba) ameungana na wanamuziki wengine waliotangulia kuingia katika tasnia ya filamu na kuweza kuigiza katika filamu kadhaa, H. Baba yeye ametoa filamu ya Promoter huku akiwa ni mtayarishaji na muigizaji katika filamu hii ya Promoter, H. Baba anaungana na wanamuziki waliotangulia kuigiza Abas Hamis Kisanza (20%), Chege Chigunda na wengineo kwa mwaka huu.

“Nimetoa filamu hii ya Promoter kwa sababu ya shuruba tunazokutana nazo sisi wanamuziki katika show zetu, kwa sababu mimi ni msanii nikatafuta njia ya kufikisha ujumbe, maana kama ni katika muziki tumesema sana, lakini jamaa bado wanaendeleza mambo yao kitapeli, kupitia filamu hii ya Promoter utapata majibu” Alisema H. Baba.

Filamu hii ya Promoter imeshirikisha wasanii wengine mahiri katika fani hii ya uigizaji kama Yusuf Mlela, Husein Mkiyeita aka Sharobaro, na mwanamuziki mwingine wa Bongo fleva Hussein Machozi, ujio wa filamu hii unafanya tasnia ya filamu Bongo kuwa kama Hollywood ambapo mastaa wengi wa muziki ucheza filamu na kuwa ni sehemu ya kujiongezea maslahi zaidi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging