Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU INAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA

Mtayarishaji wa filamu  Chrissent Mhenga  amesema kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa ili ilete tija na maslahi kwa watayarishaji na wasanii kwa ujumla, Chriss ameyasema hayo wakati akijiandaa kuandaa filamu mpya inayotarajia kuwashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu Chriss ambaye ndiye mwasisi wa kizazi kinachotamba katika filamu ameamua kuingia rasmi katika filamu. “Ukweli haupingiki kuwa wasanii wote nyote wametoka katika kundi la Kaole ambalo mimi nilikuwa Mkurugenzi wake, na niliweza kuwajenga na wameweza kuliteka soko la tasnia ya filamu hivi sasa lakini kuna jambo moja tu ambalo naliona ni matatizo ya hadithi hazishiki watu kwa muda mrefu tofauti na awali nilipokuwa nikiandikia wasanii hawa katika kundi la Kaole Sanaa Group,”anasema Uncle Chriss. Muongozaji huyo wa filamu hapa nchini ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Mega Video amekusudia kuanza kurekodi filamu mpya baada ya filamu yake ya kwanza ya Hazina ya Marehemu kufanya vizuri na kupata maoni mengi kutoka kwa wadau wengi, lakini anawasisitizia wasanii kujitahidi kujifunza vitu vya kitaaluma kwani hata filamu nyingi zimekuwa zikikosa uhalisi kwa kukosa taarifa kwa wahusika. 

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging