Katika onesho hilo, watu 100 wa kwanza watapata bia moja bure ili kuwafanya wapate wafurahie muziki wa bendi hiyo utakaokuwa unaporomoshwa ukumbini hapo.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga alisema mashabiki watapata burudani ya nguvu kutoka kwao, hivyo ni wakati wao kuingia kwa wingi kushuhudia onesho hilo. Alisema FM Academia ni bendi imara yenye mashabiki lukuki, hivyo wanaamini watafurahia burudani itakayoporomoshwa na bendi hiyo chini Rais wake Nyoshi el Saadat.
“Mashabiki wetu waje kwa wingi katika shoo yetu ili wapate burudani ya nguvu itakayopambwa na nyimbo zetu mpya na zile za zamani ambazo zipo kwenye kiwango cha juu.