Jacob Stephen ‘JB’ na gwiji la uchekeshaji Afrika Mashariki Amri Athuman ‘King Majuto’ wanakutana katika filamu ya Nakwenda kwa Mwanangu, filamu hiyo imetayarishwa na kampuni ya filamu ya Jerusalem ya Jijini Dar es salaam. Msemaji wa kampuni inayosambaza filamu hiyo Mbasha Kilanya amesema kuwa watakaonunua filamu hiyo watafurahia muunganiko wa wasanii hao wawili ambao ni nyota katika tasnia ya filamu “Filamu ya Nakwenda kwa Mwanangu ni filamu ya kipekee ambayo imebeba ujumbe mzito katika jamii, lakini si hilo tu bali pia unapata ladha mbili kwa wakati mmoja kwani King Majuto ana vitu vyake na JB naye kama unavyomjua katika filamu alivyoshika soko la filamu kwa sasa, lazima filamu hiyo ikimbize sokoni,”anasema Mbasha.Wasanii hawa wanakutana na kutengeneza filamu kwa mara nyingine toka walipokutana katika filamu siku za nyuma walipoigiza katika filamu ya Brother, filamu ya Nakwenda kwa Mwanangu ipo madukani...
KWA HISANI YA FC
KWA HISANI YA FC








