Google PlusRSS FeedEmail

DIBLO DIBALA GWIJI LA KUCHARAZA GITAA



Miaka ya 80 hadi 93, ni kipindi ambapo kilikuwa kinasisimua kiburudani , hali hiyo ilikuwa inatawala kizazi kipya cha muziki wa 'Soukous' kutoka nchini zaire(sasa DRC ) hasa baada ya kumalizika kwa enzi ya za akina Luambo Makiadi (Franco)

Ikumbukwe kipindi hiko miongoni mwa wanamuziki waliokuwa wakitamba ni kama Aurus Mabele, Lokasa ya Mbongo, 'Mzee Benz' Bozi Boziana, Scola Miel na mtindo wao wa Nzawisa

Utamu wa sauti kutoka kwa Lucian Bokilo na utundu wa kucharaza gitaa wa Dally Kimoko ulitosha kabisa kupagawisha watu mpaka wanasahau kama kuna kesho

Kwa wale ambao walikuwa wapenzi wa kwenda viwanja ikumbukwe kipindi hicho kiwanja kilichokuwa kikitamba ni Tazara Hostel ambapo wakati muda fulani watu wameshaanza kuchoka anapandishwa hewani 'Mzee wa Fujo' Alan Kounkou na baada ya sekunde kadhaa Jean Baron anaingia na kibao chake cha 'Mami Lolo'

Hata hivyo huwezi kuwazungumzia wanamuziki hao bila ya  kuligusia gwiji la kucharanga gitaa, Diblo Dibala, ambapo kwa kawaida anafahamika kama Diblo au kwa jina lingine 'Machine Gun' kutokana na kasi yake ya kucharaza gitaa

Historia inaonesha kuwa Diblo alizaliwa mwaka 1954 mjini Kisangani na baadae akahamia katika mji wa Kinshasa wakati huo alikuwa mtoto

Tunaelelzwa kuwa akiwa na umri wa miaka 15, alishinda mashindano ya kusaka vipaji ambapo kutokana na umahiri wake wa kucharaza gitaa ulimfanya ajiunge na bendi ya marehemu Franco, TPOK Jazz

Hata hivyo alikaa na kundi hilo kwa muda mfupi na baadae akaenda kushilikiana na makundi ya Vox Afrika, Orchestra Bella mambo na Bella Bella ambapo bendi yake ya kwanza ilikuwa ya Kanda Bongo Man

Mwaka 1979 alihamia mjini Brussels, Ubelgiji kabla ya mwaka 1981 kujiunga na bendi ya Kanda Bongo Man mjini Paris Ufaransa amabapo alifyatua albamu yake ya kwanza mwaka huo na kuipa jina la Lyole

Tangu kipindi hicho Diblo alizidi kupanda chati hususani baada ya kufanya kazi na wanamuziki kama Pepe Kale na makundi mengine mengi yaliyokuwa yakipiga muziki wa Soukous

Mwaka 1980 aliamua kuunda bendi yake aliyoipa jina la Loketo ambapo alikuwa akishirikiana na mwanamuziki Aurlus Mabele , hata hivyo miaka michache baadaye bendi hiyo ilivunjika hali ambayo ilimlazimu mwaka 1990 kuunda kundi jipya alilolipa jina la Matchatcha, ambalo hadi sasa linaendelea kufanya kazi baada ya kulifanyia marekebisho mbalimbali

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging