Google PlusRSS FeedEmail

HALI YA VENGU BADO TETE



Hali ya Joseph Shamba 'Vengu' ambaye ni msanii kikundi cha vichekesho cha Orijino Komedi bado si nzuri, na hakuna uwezekano wa kurejea katika maonesho ya kundi hilo hivi karibuni

Hayo yamebainishwa na kiongozi wa kikundi hicho Issaya Mwakilasa, 'Wakuvanga' katika mahojiano maalum ya mtandao wa Millardayo wiki hii

Wakuvanga alisema Vengu alirejeshwa nchini hivi karibuni akitokea India alikopelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini kutokana na matatizo yake makubwa hajapata nafuu

"Ukweli niwe muwazi kwa afya yake na tatizo alilonalo tunazungumzia tatizo la mshipa wa fahamu, ubongo hayo matatizo yanachukua muda mrefu" alisema Wakuvanga

"Ukiwaambia watanzania kwamba atarudi hivi karibuni tunakuwa tunajidanganya na pia watanzania wote ndiyo maana siku zote tunasema ukiwa na nafasi ya kumuombea mtu unayempenda muombee mi siwezi kuahidi kwamba labda atarudi mwezi ujao au mwaka ujao"

Alipoulizwa iwapo watamtafuta mtu mwingine kwa ajili ya kuziba nafasi ya Vengu, Wakuvanga alisema wataendelea kutumia jina lake hadi mwisho wa kikundi hicho

"Sisi kwetu tuko ofauti tumeapa ndivyo tutakavyoishi tupo saba mpaka tutakapokufa, kuongezeka kwa mtu labda sisi tukae pembeni tuwatafute watu wengine lakini tutaendelea kuwa saba hata maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi mara nyingi tunaishi tuko saba, akipungua mmoja bado tuko saba" alisisitiza msanii huyo ambaye ameamua kujitosa kwenye fani ya muziki kwa sasa

This entry was posted in

One Response so far.

  1. Anonymous says:

    HAKIKA UMENENA HUO NDIO UJAMAA ALIOAMINI NYERERE NA KAWAWA MUNGU AWAREHEMU

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging