Jina lako halisi ni nani?
Recho: Jina nililopewa na wazazi wangu ni Rachael Haule, na la kisanii ni 'Recho' natumia hili zaidi ili kujitambulisha mimi mwenyewe na kazi zangu
Umezaliwa mkoa gani & mwaka gani?
Recho : Nimezaliwa mkoa wa Kigoma mwaka sitopenda kuuweka wazi
Kiwango chako cha elimu
Recho : Nilisoma mkoani Kigoma ila niliweza kuishia kidato cha tatu, sikuweza kumaliza shule kwa sababu mbalimbali ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu, ila ninamshukuru mungu ninaweza kumudu maisha yangu ka elimu ndogo niliyoipata
Mtoto wa ngapi katika familia yenu?
Recho : Mimi ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wa wili wa mzee Haule , kwa kifupi mimi ni( kitinda mimba) nikimaanisha ni mtoto wa mwisho
Je wewe ni kabila gani ?
Recho : Mimi ni Mmanyema
Utamaduni wa kabila yako ni nini?
Recho: Ki ukweli sifahamu utamaduni wa kabila yangu, labda ni kwa sababu sijakaa sana mkoani
Unataka kitu gani kukifanya kwa kipindi hiki cha miezi mitatu?
Recho : Ni kutoa video ya wimbo wangu mpya wa 'Nashukuru' naamini utafanya vizuri katika gemu hili la muziki
Ni kitu gani unachokipenda kukifanya wakati huna kazi???
Recho : Napenda kushinda studio mara nyingi kama sina kazi ya kufanya, huku nasikiliza muziki na kutengeneza mawazo mapya wa muziki wangu na kunifanya nizidi kukuwa katika tasnia hiyo ya muziki
Unapenda mtindo gani ya nywele?
Recho : Napenda mtindo wa 'crazy' huwa unanifanya nionekane vizuri na kuzidisha urembo wangu zaidi
Je umeshawahi kushirikishwa kwenye kazi yoyote?
Recho : Nimewahi kushirikishwa na nyimbo ilitoka ila haikufanya vizuri
Nini unachokiangalia zaidi katika sekta ya muziki wa Tanzania?
Recho : Naangalia muziki unaelekea wapi na mimi kuufwata muziki na si muziki kunifuata, namaanisha kuwa msanii unatakiwa ubadilike kulingana na mazingira na soko la muziki linataka nini,
Ni kitu gani unakikumbuza zaidi na kwa nini ?
Recho : Nakumbuka zaidi nilivyoanza kazi ya muziki yaani wazazi wangu walikuwa hawataki mimi niwe msanii na nilikuwa siwaelewi kabisa kwani nilikuwa ninapenda kuimba na kuwa msanii
Nini baadhi ya malengo yako ya baadae?
Recho : Kuwa mwanamuziki na siyo kuwa tena Recho, niwe ninauwezo mkubwa wa kufanya kazi nzuri zilizojaa ubunifu ndani yake
Mbali ya muziki unafanya kitu gani cha kuongeza kipato ?
Recho : Bado sijaanza kujihusisha na kitu chochote kile kwa sasa ninaukazania muziki wangu ili niweze kutimiza malengo yangu
Umeshatoa Albamu na kama bado unampango gani ?
Recho : Bado sijatoa albamu ila ninaandaa albamu yangu ya kwanza kwa sasa nina 'single' tatu, Upepo, Kizunguzungu na Nashukuru hizo ndizo nyimbo zangu ambazo zinasikika katika vituo vya radio mbalimbali
Unafikiria ni sehemu gani ya mwili wako ni bora na inakufanya uwe na mvuto ?
Recho : Sura yangu kiujumla ikiwa inazidishwa na macho yangu makubwa mazuri yanazidi kunionyesha ninamvuto na ni bora katika mwili wangu, pamoja na shepu yangu nzuri iliyoumbika vizuri inayosababisha nionekane vizuri ninapovaa nguo zangu
Jinsi gani unaweza kuelezea ulivyo kwa jamii?
Recho : Mimi ni mtu wa kawaida, mpole ninayependa kuzungumza na watu wa rika tofauti tofauti ninayependa kucheka, sina tabia ya kununa ovyo na huwa siipendi
Je ni kitu gani kuhusu wewe jamii ikisikia watashangazwa kujua ?
Recho : Napenda kudega ghafra tabia hiyo ninayo sana hata nikiwa nimekaa na marafiki zangu wakawaida tu huwa najikuta tabia hiyo ya kudeka ghafra inatokea
Unapenda mahusiano ya namna gani ?
Recho : Napenda ,mahusiano ya kipekee na si ya kuigiza, unamuona mtu yuko na mahusiano ya namna fulani na wewe unataka kuwa kama wao, hayo mimi siyapendi napenda mahusiano ya kipeke
Mwaka gani uliumizwa na mahusiano?
Recho : Ni mwaka huu tena hivi karibuni mwezi wa 8 niliumizwa sana na mahusiano na sipendi kuyaongelea








