Google PlusRSS FeedEmail
Muimbaji Rihanna ambaye haishi vituko kila siku atoa kali ya mwaka baada ya kupozi huku sehemu kubwa ya mwili wake ukiwa unaonekana

RIHANNA AENDELEA KUWA KITUKO

Muimbaji Rihanna ambaye haishi vituko kila siku atoa kali ya mwaka baada ya kupozi huku sehemu kubwa ya mwili wake ukiwa unaonekana [Read More]


Mwanamitindo Heidi Klum ameushangaza ulimwengu baada ya kwenda mtoko huku akiwa amevalia ndala Heidi ni mmoja wa wanamitindo wenye heshima kubwa duniani ambaye asili yake ni Mjerumani

Mwanamitindo huo alionekana na ndala hizo zenye mkanda mweusi akielekea katika mgahawa wa Nobu kwa ajili ya kupata chakula cha usiku na mpenzi wake Martin Kristen huko New York

MWANAMITINDO AONEKANA NA NDALA

Mwanamitindo Heidi Klum ameushangaza ulimwengu baada ya kwenda mtoko huku akiwa amevalia ndala Heidi ni mmoja wa wanamitindo wenye heshim... [Read More]


Baada ya kuathirika kwa muda mrefu na dawa za kulevya hatimaye mwanamitindo mwenye heshima kubwa duniani Naomi Campbell amerudi tena kwenye gemu

Naomi katika miaka ya hivi karibuni alikumbana na matatizo mengi yaliyotokea na matumizi ya kupitiliza ya dawa za kulevya hali iliyopelekea kukosa dili mbalimbali

Hivi karibuni mwanamitindo huyo alionekana katika onyesho la mavazi akiwa na Kate Moss ambaye walivaa nguo za kufanana

NAOMI CAMPBELL AREJEA KWENYE GEMU

Baada ya kuathirika kwa muda mrefu na dawa za kulevya hatimaye mwanamitindo mwenye heshima kubwa duniani Naomi Campbell amerudi tena kwen... [Read More]


Mwanamuziki wa Pop Chris Brown ameanzisha vita vya maneno na Miss Urusi baada ya kumwita mwanamke huyo malaya.

Brown hivi karibuni aliripotiwa kuwa na mahusiani ya kimapenzi na Olga Gure Kovalenko ambaye ni Miss Urusi 2013, lakini msanii huyo aliibuka na kudai kuwa hakuwa na haja na binti huyo zaidi ya kumchukulia kama malaya na alimytaka kwa ajili ya kufanya naye mapenzi na kumwacha.

CHRIS BROWN AMWITA MISS URUSI MALAYA

Mwanamuziki wa Pop Chris Brown ameanzisha vita vya maneno na Miss Urusi baada ya kumwita mwanamke huyo malaya. Brown hivi karibuni alir... [Read More]


Serikali kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani.

taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za kitanzania, imeeleza kuwa aunt aliipeleka filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania.

“kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina.


kabla ya mwandishi wetu hajazungumza na aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.


“amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa aunt kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.

alipotafutwa aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.



mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji vincent kigosi ‘ray’ kuingiza sokoni sinema ya sister mary baada ya kuridhishwa na madai ya kanisa katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha ukatoliki.

FILAMU YA AUNT EZEKIEL YAZUILIWA BAADA YA KUWA NA VIPANDE VYENYE KUCHOCHEA NGONO

Serikali kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya i... [Read More]


MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka ashangazwa na baadhi ya wasanii wa filamu kujichubua ili kujiongezea urembo bila ya kujali kuharibu ngozi zao.

Mshangao huo umeibuka baada ya baadhi ya mashabiki wa filamu kushangazwa na muonekano wa baadhi ya wasanii kubadilika siku hadi siku.

Rose aliweka wazi kuwa chanzo cha kujichubua kwa baadhi ya wasanii hao ni kutaka kuongeza urembo katika muonekano wao huku wakiamini kuwa njia ya kuwa mrembo ni kujichubua.

Alisema kuwa kujichubua si njia sahihi ya kuongezea urembo bali ni njia ya kuendelea kujiharibu na kuonekana mzee hata kama umri wako ni mdogo.

"Mimi nawashangaa sana wanatafuta uzuri kwa njia ya kujichubua mimi sipaki mkorogo lakini bado niko vizuri na naonekana mrembo pia., hivyo kujichubua si kuongeza urembo waelewe hivyo" alisema Rose

Aliweka wazi kuwa baadhi ya wasanii wengi wanamuonekano tofauti na walivyoanza kazi yao ya sanaa, kutokana na mikorogo wanayoitumia.

ROSE NDAUKA ASHANGAZWA NA BAADHI YA WASANII KUTUMIA MIKOROGO

MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka ashangazwa na baadhi ya wasanii wa filamu kujichubua ili kujiongezea urembo bila ya kujali kuharibu n... [Read More]

  Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu, kwa hiyo kwa kuwa nao si rahisi kuonyesha mapenzi yao ya dhati kwake kwani mapenzi yao ni chumbani tu, lakini hawezi kutembea nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake alafu mtu mzima hivi unakosa penzi la kweli kwani mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni wapenzi lakini ukiwa na kijana ambaye ni rafiki hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyesha jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake”,

“Wengi watu wenye pesa zao kuna wakati wananiona nina dharau lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke ya mtu anayenijali na kuwa karibu na mimi sasa kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe.

Aidha kuna watu ambao uwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu wengine wao si malaika wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.

MAPENZI YA KWELI NDIO MPANGO MZIMA PESA BAADAE

  Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi w... [Read More]

Omary Fereji Nyembo - Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya Dmk Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine baran Ulaya."yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa Dmk Global Promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz
nilipomuuliza kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema " unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa?

DIMPOZ KUKIMBILIA MAREKANI

Omary Fereji Nyembo - Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya Dmk Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na ... [Read More]

VAZI LA SUSPENDER NDANI YA FASHION

[Read More]


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi 'Afande Sele' amuombea msamaha msanii wa muziki Omary Faraja 'Ommy Dimpozi' kutokana na kauli yake aliyeitoa inayodaiwa kumkashifu marehemu Alberty Mangwea 'Ngwair'.

Msamaha huo umetokana na kauli aliyeitoa msanii Ommy Dimpozi kudai kuwa hawezi kufa maskini kama msanii Ngwair.

Afande Sele alidai kuwa kauli hiyo haikuwa mbaya ingawa watanzania hawakuilewa hivyo Ommy ametereza ulimi na anapaswa kusamehewa kama binadamu anapokosea.

Alisema kauli yake ilikuwa inamaanisha wasanii wanatakiwa wapate haki za msingi na siyo kutumiwa huku wengine wakiendelea kunufaika na wao kudidimia na hali ngumu ya kimaisha.

"Hatuwezi kuendelea kufanya hivyo mimi namuombea msamaha kwa watanzania kauli yake ilikuwa na lengo zuri ila ameshindwa kuifikisha vyema hivyo ameteleza inabidi tumsamehe ili mambo mengine yaendele" alisema Sele.

Wakati huo huo bado ile  kauli anayodaiwa kuitoa msanii huyo Ommy Dimpozi' inaendelea kumtesa na kusababisha kushindwa kuwapa burudani mashabiki zake.

Ommy  Dimpozi alipata wakati mgumu baada ya kufanyiwa fujo na mashabiki alipokuwa akifanya shoo pamoja na wasanii wenzake walioshiriki katika Tuzo za Kilimanjaro mwaka huu wakiwa mjini Dodoma.

Msanii huyo anadaiwa kutoa kauli hiyo hivi karibuni ambapo alisema hataki kufa masikini kama ilivyokuwa kwa msanii wa Hip hop Albert Magwear.

Kauli hiyo iliwachukiza baadhi ya mashabiki wa muziki waishio mjini Dodoma ambapo msanii Magwear alisoma na kukulia katika mji huo.

Msanii huyo atazidi kuwa na wasiwasi kwa baadhi ya mikoa atakayozunguka kufanya shoo zake ikiwemo mkoa wa Morogoro ambapo ndio familia ya msanii huyo inapoishi.

Alipotafuta na mwandishi wa habari hili kuzungumzia ishu hiyo Dimpozi alisema hayuko tayari kusema chochote kinachohusiana na shoo yake ya Dodoma na hataki kumzungumzia Magwear.




AFANDE SELE AMUOMBEA MSAMAHA DIMPOZI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi 'Afande Sele' amuombea msamaha msanii wa muziki Omary Faraja 'Ommy Dimpozi... [Read More]


Baada ya ukimya wa muda mfupi msanii wa miondoko ya Hip Hop Gosby ametoa nafasi kwa wasichana watatu watakaoweza kujibu maswali yanayohusu muziki wake kwa ufasaha kwenda kusikiliza kwa mara ya kwanza wimbo wake mpya alioupa jina la 'Baby Making Swag aka BMS' siku ya Jumatano (leo) kwenye studio za B'Hits zilizopo Kawe.

Aliweka wazi kuwa ameamua kuwachagua  wasichana pekee yake kwa sababu mahadhi na ujumbe unaopatikana kwenye nyimbo hiyo unawagusa wasichana zaidi.

Mbali na hilo pia ameamua kuwafanya wasikilizaji wake kuwa wa kwanza kuusikiliza muziki huo, huku akitarajia kupata ushauri kupitia mashabiki wake.

GOSBY AJA NA EXCLUSIVELY KWA MABINTI

Baada ya ukimya wa muda mfupi msanii wa miondoko ya Hip Hop Gosby ametoa nafasi kwa wasichana watatu watakaoweza kujibu maswali yanayohus... [Read More]


Mwanamuziki Kelly Rowland ambaye ni mmoja miongoni wa wadada wanaounda kundi la Destin Child ametoa ya moyoni kitu kinachomkera ambacho Beyonce anacho kuwa ni uvivu na uzembe

Akizungumza katika mahojiano maalumu Kelly alisema kuwa Beyonce anamambo mengi na anajua vitu vingi lakini suala la uvivu ndilo linamsumbua

Kelly aliweka wazi kuwa anamjua Beyonce muda mrefu kutokana na kufanya naye kazi na anajua uwezo wake wa kazi ingawa hataki kujituma zaidi ya hapo

BEYONCE ASUMBULIWA NA GONJWA LA UVIVU

Mwanamuziki Kelly Rowland ambaye ni mmoja miongoni wa wadada wanaounda kundi la Destin Child ametoa ya moyoni kitu kinachomkera ambacho B... [Read More]


"PICHA ni moja ya jambo linalofikisha habari kwa jamii,picha inaweza kusimama pekee yake na ukagundua nini kinachozungumzwa" hayo ni maneno yanayosemwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Jumaa Mohamedy 'Jaymoe Mchopanga' na mwandishi wa habari hii.

Jaymoe mbali ya kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya pia anajishungurisha na maswala ya upigaji picha huku akiamini kuwa siku moja kuwa mpiga picha wa kimataifa.

Jaymoe anaamini kuwa mpiga picha bora anauwezo wa kutengeneza video bora kwa upande wa muziki, hivyo kutokana na juhudi zake za kuwa mpiga  picha bora anaamini ataleta mageuzo katika upande wa utengenezaji wa video za muziki hapa nchini.

Jaymoe ambaye anahisi kukosekana kwa wapigapicha bora ndio inapelekea kukosa video zenye ubora tofauti na nchi jirani ambapo wao kwa upande wao wameweza kufanya vizuri kwa upande huo.

Anaamini kupitia kitengo cha kupiga picha atafanikiwa kuwa mtengeneza video bora za muziki ambapo hivi sasa anahisi baadhi ya video hizo hazitendewi haki kutokana na kukosa ubora.

Jaymoe ambaye ameanza safari yake ya muziki alipokuwa shule ya sekondari ingawa aliweza kujulikana kwa jamii mnamo mwaka 2001 baada ya kundi la wateule kukubalika kwa jamii.

Jaymoe ambaye ametokea katika kundi la wateule, aliweza kushirikishwa na kutokana na nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Ulingoni' ambayo ilibeba jina la albamu ya kwanza ya msanii Solo .

Jaymoe ambaye aliweza kuikamilisha albamu yake ya kwanza akiwa chini ya studio za Bongo Records huku P- Funk akiwa ni mtayarishaji wa nyimbo zake ambapo nyimbo ambayo ilizidi kumpa umaarufu ilijulikana kwa jina la 'Mvua na Jua' .

Single ya Maisha ya Boding ni nyimbo ambayo bado inaendelea kumpa umaarufu Jaymoe ambapo kilichoimbwa katika nyimbo hiyo ni ualisia wa maisha wanayoishi wanafunzi wengi waishiyo boding.

Jaymoe ambaye mara nyingi hupenda kutumia zaidi muda wake akiwa nyumbani na siyo kutoka anaamini kuwa kusihi ndani huku akitumia computar kwa ajili ya kuongeza vitu tofauti tofauti ni njia pekee inayomuondoa na makundi mbalimbali ambayo anahisi yanaweza kuhatarisha maisha yake kwa kuiga vitu visivyofaa.

Jaymoe ambaye anamini zaidi kuvaa nguo zenye rangi ya kuvutia huku akiwa makini na fashion anaamini kuwa kupendeza ni moja ya kuongeza mvuto na muonekano sahihi., Jaymoe hajabahatika kuoa wala kupata mtoto ingawa kwa sasa anatamani kupata mtoto

JE JAYMOE KUACHANA NA MUZIKI, KUWA MPIGA PICHA??

"PICHA ni moja ya jambo linalofikisha habari kwa jamii,picha inaweza kusimama pekee yake na ukagundua nini kinachozungumzwa" ha... [Read More]


Ikiwa zimebaki siku chache kwa mwanamuziki wa Marekani miondoko ya Hip Hop Jay Z kuiachia albamu yake iliyoipa jina la 'Magna Carta Holy Grail' ameanza kwa kutoa mashairi  yanayopatikana  katika albamu hiyo

Jay Z kwa kuanza ametoa mashahiri ya wimbo unaoitwa 'Holy Grail' aliomshirikisha Justin Timberlake ambapo pia utapatikana katika albamu hiyo

JAY-Z AONJESHA UTAMU WA ALBAMU YAKE

Ikiwa zimebaki siku chache kwa mwanamuziki wa Marekani miondoko ya Hip Hop Jay Z kuiachia albamu yake iliyoipa jina la 'Magna Carta H... [Read More]


KITENDO cha Kim Kardashian kupata mtoto wa kike, huku mtoto huyo amepewa jina la North huenda kimemvutia zaidi mchumba wake Kanye West na kuamua kutangaza ndoa ambayo itafungwa hivi karibuni.

Kanye ameamua kutangaza  rasmi ndoa yake na mwanadada Kim Kardashian ingawa hajamvalisha pete ya uchumba.

Hatua ya Kanye kutangaza ndoa ya mama wa mtoto imekuja siku chache baada ya ndoa ya Kim na aliyekuwa mume wake Kris Humphries kufikia tamati rasmi kisheria wiki iliyopita baada ya mvutano wa muda mrefu na Kris waliyekaa kwenye ndoa kwa siku 72 kabla ya Kim hajaomba talaka Octeber 2011.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun inadaiwa kuwa mastaa hao wanategemea kufunga ndoa yao mwezi September mwaka huu jijini Paris, Ufaransa

KIM KARDASHIANA KUFUNGA NDOA NA KANYE WEST

KITENDO cha Kim Kardashian kupata mtoto wa kike, huku mtoto huyo amepewa jina la North huenda kimemvutia zaidi mchumba wake Kanye West na... [Read More]


KATIKA fani ya muziki wa kizazi kipya nchini  hauwezi kuuzungumzia muziki huo bila ya kumtaja prodyuza mahiri Paul Matthysse  'P- Funk Majani, kutokana na juhudi zake za  kuutambulisha muziki huo kwa jamii.

P- Funk ambaye ni mmiliki wa studio ya Bongo records iliyopo jijini Dar es Salaam ameweza kuwapika wasanii wengi wa muziki huo wa kizazi kipya walio maarufu nchini.

Mtayarishaji huyo wa muziki wa kizazi kipya miaka 22 iliyopita alionyesha hisia za kuupenda muziki na kuuendeleza nchini kutokana na hali hiyo ilimsukuma kuinua vipaji vya wasanii walio wengi ambao hadi hivi sasa wanafanya vizuri kwenye gemu hilo huku historia ikionyesha kuwa wamepitia mikononi mwa P- Funk.

Mbali na kuwa na kipaji cha kuutengeneza muziki pia aliweza kwenda masomoni ambapo alijifunza mambo mbalimbali yahusio muziki, 'Sound Engineering' kwa muda usiopungua mwaka mmoja.

Kutokana na ndoto za kutaka kuinua muziki wa kizazi kipya nchini P-Funk baada ya kusomea mambo yahusiyo muziki, mnamo mwaka 1995 aliweza kuanzisha lebo yake pamoja na kufungu studio iliyopewa jina la Bongo Records.

Akiwa bado ni prodyuza mchanga studio yake ya bongo records ilianza kupata umaarufu, kwa kipindi hicho neno la 'bongo' lilikuwa ni moja ya neno la kiswahili linalovuma na ndipo Albamu  ya Bongo Dar es Salaam ilipozinduliwa .

Kwa kipindi hiko akiwa bado ni mtayarishaji mdogo alifanikiwa kupata umaarufu mkubwa katika fani ya muziki na hasa katika mlipuko wa nyimbo za bongo fleva.

KUUTAMBULISHA MUZIKI KWA JAMII.

Mtayarishaji huyo aliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuutambulisha muziki huo na kuufanya ukubariki kwa jamii nzima huku akipambana na ugumu wa mapokeo ya muziki huo kwenye jamii ambapo baadhi ya wazazi waliamini kuwa muziki ni uhuni.

P-Funk  aliweza kuandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kutafuta vijana wenye vipaji na kuingia nao mkataba wa kufanya nao kazi katika lebo yake, alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kupata vijana wenye uwezo wa kuimba na kufanya nao kazi katika mazingira ya muziki.

Haikuwa kazi raisi kwake kuishawishi jamii kukubali kuupokea muziki wa bongo fleva kama  ni moja ya njia ya kujiajili, kutokana na kuupenda muziki na kuhitaji mafanikio ya muziki wa kizazi kipya nchini aliweza kutumia njia ya ziada ambapo jamii iliweza kuupokea  muziki huo na kuutambua kama ni njia moja wapo ya kujiajili.

P- Funk kwa kupitia  'talent shoo' aliweza kuibua vipaji vya wasanii chipukizi na vijana waliowengi kutambua vipaji vyao pamoja na kuingia katika ushindani wa vipaji walivyonavyo huku kila mmoja akiwa na kiu ya kufikia mafanikio ya kuwa mwanamuziki bora.

Kupitia Talent shoo alizozifanya na kuibua vipaji vya wasanii wachanga na baadhi ya vijana wengine kupata mafanikio ya muziki aliweza kubadili fikra za jamii na kuupokea muziki kuwa ni sehemu ya ajira na si uhuni kama hapo awali walivyofikiria.

WASANII ALIOWAINUA.

Mtayarishaji huyo kupitia mikono yake aliweza kuleta mageuzi katika tasnia hiyo ya muziki na kufanikiwa kuibua vipaji vya wasanii akiwemo Juma Nature, Solo Thang, Zay B, Sista P, Professor Jay, Lady Jaydee, ikiwa hao ni baadhi ya wasanii aliowainua kwenye maswala ya muziki.

P -Funk aliweza kumpandisha chati Juma Nature ambaye ni nyota wa muziki wa kizazi kipya, aliweza kufanikiwa zaidi alipotoa albamu yake inayojulikana kwa jina la 'Ugali' ambapo kutokana na umahili wa kushuka mistari msanii huyo iliweza kupewa vionjo na uwezo wa mtayarishaji huo kwa kutengeneza midundo yenye ujazo wa hali ya juu ambayo iliweza kufanikisha kwa kiasi kikubwa nyimbo hizo kufanya vyema katika tasnia ya muziki huo.

Mtayarishaji huyo pia ameweza kuweka rekodi ya kipekee katika tasnia ya muziki kwa kufikisha mafanikio makubwa ya uzinduzi wa albamu hiyo ya Ugali ambapo Juma Nature aliweza kufanikiwa kufanya uzinduzi wa kipekee kwa kujaza ukumbi wa Diamond kwa kiwango kikubwa cha mashabiki hadi sasa hakuna msanii yeyote aliyeweza kufanikiwa kuipita rekodi hiyo iliyoachwa na mtayarishaji huyo.

Juma Nature ambaye hadi sasa ni nyota wa muziki wa kizazi kipya huku akiendelea kuliteka soko la muziki huo ni dhahiri kuwa bila uwepo wa prodyuza huyo asingeweza kufahamika msanii huyo, P- Funk ananafasi ya kipekee kwa kuinua vipaji pamoja na kuendeleza muziki wa kizazi kipya.

Mbali na Juma Nature, aliweza kumtambulisha kwenye gemu marehemu Albert Mangwea 'Ngwair', ambaye kutokana na umahili wake wa kutambua vipaji na kutengeneza beat aliweza kufanikisha malengo ya msanii huyo na kutambulika vyema kwenye gemu hilo la muziki.

Ngwair ambaye hakufahamu kama angeweza kupata bahati ya kuingia studio na kurekodi nyimbo ikaweza kusikilizwa P-Funk aliweza kutimiza ndoto za msanii huyo na kumuibua kama msanii bora wa Hip Hop nchini.

Albamu ya 'A.k.a Mimi' ni albamu bora ya hip hop ambayo ilipikwa mikononi mwa mtayarishaji huyo huku albamu hiyo ikimtambulisha na kumuongezea mashabiki lukuki msanii huyo kwenye gemu la muziki, huku nyimbo kama 'geto langu' bado inaendelea kufanya vizuri kwenye gemu hilo.

Bado mtayarishaji huyo jina lake linaendelea kukumbukwa kwa kipindi chote cha muziki wa bongo fleva  kwa kuwapika wasanii wengine wengi akiwemo Jaydee, Zay B, Solo Thang, Professor Jay, Jaymoe na wengine wengi bila ya kumsahau Afande Sele.

Nyimbo kama Chemsha bongo, Ugali, Mkuki moyoni, Geto langu, Mvua na Jua, Maisha ya boding hizo ni baadhi ya nyimbo ambazo zilizidi kumpa mashabiki na kila mmoja kumfwatiria mtayarishaji huyo kutokana na umahili wake katika utengenezaji wa muziki.

P funk bado anandoto ya kuendelea kufanya muziki huo kuwa na mtazamo tofauti zaidi hivyo anazidi kujipanga na kuweka mikakati iliyothabiti kwa ajili ya kupambana na changamoto mbalimbali.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii P Funk aliweka wazi kuwa sasa anajipanga kuufanya muziki kibiashara zaidi na tofauti na hapo awali ambapo aliweza kuwanufaisha wasanii wengi kupata majina na wadau mbalimbali wa muziki kufaidika kupitia kitu alichokitengeneza.

"Muziki sasa uwe na mtazamo wa tofauti inabidi tufanye muziki wa biashara zaidi sitaki kuwanufaisha watu lazima ifike hatua kila mtu apate faida kwa kile alichokifanya na siyo kunufaishana na wengine wakose mafanikio" alisema P- Funk.

Mtayarishaji huyo ambaye anaamini kipaji chake na uwezo wake aliyonao kutengeneza muziki anaamini bado ananafasi kubwa ya kuubadilisha muziki huo na kuleta muziki ambao baadhi ya mashabiki wengi wameikosa ladha hiyo.

P Funk anajipanga kuja na njia ya tofauti ya msanii kutengeneza hela na siyo kutegemea zaidi shoo kama ilivyozoeleka hivi sasa, kuwa msanii ili aweze kupata kipato chake atatumia zaidi shoo kuliko kufanya kito cha tofauti.

P Funk bado baadhi ya wasanii walio wengi wanakiu ya kufanya naye kazi huku baadhi yao wameweka wazi kuwa mtayarishaji huyo mbali na ukongwe wake wa kutengeneza muziki huo bado anajua nini anachokifanaya na kufahamu kipaji cha mwanamuziki kila anayeingia katika lebo yake.

P Funk ameweza pia kupata heshima ya muziki huo kwa kupata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya Tanzania Kilimanjaro Music Awards mwaka 2003, 2005, 2006 kama mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya, kutokana na heshima ambayo ameiweka katika tasnia hiyo bado baadhi ya taasisi zinatoa heshima kwa kumtunuku tuzo mtayarishaji huyo.

P Funk bado anahitajika kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya kwa kuwa ni mtayarishaji wa kwanza kupigania maslahi ya mwanamuziki ili aweze kunufaika na kile anachokifanya, ni miongoni mwa watu aliyekuwa anahakikisha albamu ya msanii inaingia sokoni.

Kulingana na mambo kubadilika na wasanii wengi kuuza single kwenye matumizi ya miito ya simu, P Funk bado ananafasi kubwa ya kuhakikisha wasanii wananufaika kupitia mauzo hayo kutokana na ujuzi alionao katika suala hilo la kufanya muziki kibiashara.

P- FUNK PRODYUZA ANAYEJIVUNIA KAZI YAKE

KATIKA fani ya muziki wa kizazi kipya nchini  hauwezi kuuzungumzia muziki huo bila ya kumtaja prodyuza mahiri Paul Matthysse  'P- Fun... [Read More]

Chris Brown ft Aaliyah - Don't Think They Know

[Read More]


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini miondoko ya Hip Hop, Jumaa Mohamedy 'Jaymoe Mchopanga' amewashangaa baadhi ya wasanii kutafuta umaarufu kwa kutumia madawa ya kulevya.

Akizungumza na jarida hili Jaymoe aliweka wazi kuwa anashangazwa na baadhi ya wasanii hao kutumia madawa ya kulevya hali ambayo inapelekea kushusha hadhi ya tasnia yao ya muziki wa kizazi kipya.

Alisema kuwa hapo awali tasnia hiyo iikuwa haina sifa ya wasanii kutumia madawa ya kulevya ila sasa kutokana na baadhi ya wasanii kutafuta umaarufu hivyo wanajikuta wanatumia madawa ya kulevya.

"Ni bora kuwa na mademu wengi kuliko kutumia madawa ya kulevya kwani utumiaji wa madawa hayo yanaaribu dira na mfumo wa maisha kiujumla" alisema Jaymoe.

"Hapo mwanzo fani hii ilikuwa inasifika kuwa na wasanii mabishoo lakini tofauti na kipindi hiki ambacho kumeibuka na hili tatizo la baadhi yao kutumia madawa ya kulevya huku wakiamini kuwa ili uwe bora kimuziki lazima utumie madawa hayo jambo ambalo halina tija kwenye fani yetu" alisema Jaymoe.

Pamoja na hayo Jaymoe aliongezea kuwa anampango wa kubadili mfumo mzima wa mazingira ya wasanii ili kuokoa kizazi ambacho kimejikita kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwani kwa kufanya hivyo anaamini ataokoa kizazi pamoja na muziki wa kizazi kipya.

JAYMOE ASHANGAZWA BAADHI YA WASANII WANAOTUMIA MADAWA KUTAFUTA UMAARUFU

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini miondoko ya Hip Hop, Jumaa Mohamedy 'Jaymoe Mchopanga' amewashangaa baadhi ya wasanii kut... [Read More]

BAADHI YA MASHABIKI WA PRO 24 DJ'S

[Read More]


Baada ya mashabiki wake kujiuliza maswali mengi juu ya mwenendo mzima wa tabia ya msanii kinda wa Pop Justin Bieber, ameendelea kudhihirisha kuwa ni mpenzi wa kuvuta bangi baada ya kuonekana katika picha na msokoto huo.

Bieber aliamua kutuma picha hiyo ikimuonesha na misokoto ya dawa hiyo ya kulevya katika mtandao wa instagram.

BIEBER AENDELEZA BANGI

Baada ya mashabiki wake kujiuliza maswali mengi juu ya mwenendo mzima wa tabia ya msanii kinda wa Pop Justin Bieber, ameendelea kudhihiri... [Read More]


Hatimaye Kanye West na Kim Kardashian teyari wamechagua jina la kumpa mtoto wao wa kike na kumwita North West aliyezaliwa hivi karibuni

Kim na Kanye wamepata mtoto wao wa kwanza na kuamua kumwita rasmi jina hilo huku wakidai kuwa wanapenda afupishwe jina hilo na kuitwa Nori

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia hiyo aliweka wazi kuwaa wawili hao walikubaliana jina hilo baada ya kupita siku tano za kujifungua kwa Kim

KANYE AMPA MTOTO WAKE JINA

Hatimaye Kanye West na Kim Kardashian teyari wamechagua jina la kumpa mtoto wao wa kike na kumwita North West aliyezaliwa hivi karibuni ... [Read More]



Baadhi ya picha behind the sine zinazoonyesha shoot ya video ya wimbo mpya wa Izzo B unaojulikana kwa jina la  LOVE ME ambao ndani kawashilikisha Shaa na Barnaba classic, hizi ni baadhi ya picha zilizopatikana wakati wa kushoot video hiyo



PICHA VIDEO YA LOVE ME IZZO B

Baadhi ya picha behind the sine zinazoonyesha shoot ya video ya wimbo mpya wa Izzo B unaojulikana kwa jina la  LOVE ME ambao ndani kawashi... [Read More]


Tamasha la muziki la kimataifa ambalo hufanyika kila mwaka la ‘World Music Day’ linafanyika leo (Ijumaa) katika viwanja vya posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo wanamuziki Kala Jeremiah, Ben Paul, bendi ya Twanga pepeta na wengineo wanaotamba katika tasnia ya muziki nchini watalipamba tamasha hilo.

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Umoja wa Ulaya wa taasisi za utamaduni (EUNIC) zikiwamo Aliance France-Dar es Salaam, Goethe Institut-Tanzania na British Council linalenga kutoa fursa kwa wanamuziki wakongwe na wachanga kukutana katika jukwaa hilo la kimataifa kutoa burudani hiyo kwa wapenzi na mashabiki wa muziki.

Mratibu wa Tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na Fasjet, Abel Shuma ambaye pia ni Mratibu wa Shughuli za Utamaduni Alliance France Dar es salaam amewataja wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na Msanii wa Reggae nchini Jhiko Man, Barnaba na bendi yake, Ben Paul na Twanga Pepeta

Wengine ni Msanii bora wa mwaka na msihindi wa tuzo tatu za KTMA Kala Jeremiah, Godzila, Super Maya Baikoko, Makini Kids na wengine wengi ambao watajumuika kwa pamoja kunogesha tamasha hilo ambalo hufanyika Juni 21 kila mwaka katika nchi 116.

Shuma amesema hakutakuwa na kiingilio katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanza majira ya saa kumi na moja jioni na hivyo kuwaomba wapenzi na mashabiki wa muziki kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo linalodhaminiwa na Fastjet, Balozi za Ufaransa na Ujerumani, kinywaji cha Pepsi na Total.

Kala Jeremiah analielezea onyesho hilo kama mazao ya kazi nzuri aliyoifanya katika muziki wake “Nimepata faraja sana kualikwa kutumbuiza kwenye world music day, inaonyesha ni kwa jinsi gani muziki wangu unakubalika na kutambulika kitaifa na kimataifa”.

Shirika la ndege la Fastjet kupitia kwa Afisa Masoko Mtendaji Lucy Mbogoro linajivunia kudhamini tamasha hilo likitumia nafasi hiyo kurejesha shukran kwa Watanzania kwa mchango wao mkubwa katika shirika hilo kwa kuchagua kutumia huduma zake za usafiri wa anga.

Mbogoro anasema “World Music Day ni fursa nzuri ya kukutana na wadau wetu kwakuwa tamasha litawakutanisha watu wa mataifa mengi watapata kujua huduma zetu katika wakati huu tunaoelekea kuanzisha safari za ndege za kimataifa katika nchi za Afrika Kusini, Zambia na Rwanda”


TWANGA, KALA JEREMIAH, BEN POL KUTUMBUIZA TAMASHA LA 'WORLD MUSIC DAY IJUMAA

Tamasha la muziki la kimataifa ambalo hufanyika kila mwaka la ‘World Music Day’ linafanyika leo (Ijumaa) katika viwanja vya posta Kijit... [Read More]


Baada ya kukaa kimya kwa kipindi cha muda mrefu kwa muigizaji mkongwe wa filamu maarufu za action Arnold Schwarzenegger, ameamua kurejea upya katika ulingo huo huku 'Terminator 5' inategemea kurekodiwa mwezi January mwaka ujao.

Hii itakuwa ni mara ya 4 kwa mcheza filamu huyo kushiriki katika movie hiyo baada ya kushindwa kushiriki katika Terminator 4 kutokana na majukumu ya u-Governor wa Califolirnia kwa wakati inatengenezwa

ARNOLD SCHWARZENEGGER NDANI YA 'TERMINATOR' 5

Baada ya kukaa kimya kwa kipindi cha muda mrefu kwa muigizaji mkongwe wa filamu maarufu za action Arnold Schwarzenegger, ameamua kurejea ... [Read More]


 MSANII wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee kivazi chamuumbua katika tuzo za Tanzania Kilimanjaro Music Awards zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo alijikuta akishindwa kutembea huku akijiziba mbele kutokana na kigauni alichokuwa amevaa kuwa na mipasuo huku kukiacha sehemu kubwa ya mwili wake.

Vanessa alionekana kuwa na wasiwasi kila alipopanda jukwaani huku akiziba mipasuo ya nguo yake ili kuepusha aibu ya kuonyesha mapaja yake kutokana na mipasuo ya kivazi hicho.

Baadhi ya watazamaji waliofika ukumbini hapo walionekana kushangazwa na kitendo hiko huku wengine wakiohoji kwa nini ameamua kuva hivyo huku akipata wasiwasi wa kuficha sehemu ya mwili wake ili usionekane.

"Kwa nini ameamua kuvaa gauni hilo wakati anajua lina mipasuo mirefu ni bora angeacha tu kuliko hivyo anavyopata shida nalo kwa kulishika kuzuia hiyo mipasuo" alisema mdau mmoja aliyehudhuria tuzo hizo.


VANESSA KIVAZI CHAMUUMBUA TUZO KILIMANJARO

 MSANII wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee kivazi chamuumbua katika tuzo za Tanzania Kilimanjaro Music Awards zilizofanyika mwishoni ... [Read More]







Mtanzania mwenzetu anaye tuwakilisha kwenye jumba la Big Brother katika shindani la 2013 Big Brother Africa 8 The Chase "Nando" amewekwa kwaajili ya kutolewa.

Ni kura yako tu ndio itakayomuokoa kuondolewa ndani ya jumba hilo. tafadhali ukiwa kama Mtanzania mwenye uzalendo na nchi yako mpigie kura Mtanzania mwenzetu ashinde kwa kutuma sms mara nyingi uwezavyo.

Kumuokoa piga kura kwa kutuma sms ifuatavyo:-
* Sms - jina Nando kwenda 15456
* Temebelea website
www.bigbrotherafrica.com<http://www.bigbrotherafrica.com> na uingize maelezo yako kisha chagua VOTE & WIN itakupa orodha ya majina ya waliowekwa kwenye orodha ya kuondolewa.


Mpigie kura Nando

Kumbuka kwamba unaweza kupiga kura kila mara moja kwa kila saa moja, piga kura mara nyingi uwezavyo.

Watanzania tunaweza...
Tuhamasishane marafiki, ndugu, jamaa majirani na watanzania wote kupiga kura mara nyingi iwezekanavyo kumuokoa mwenzetu NANDO

PIGA KURA "Nando" KWA NAMBA ZIFUATAZO HAPO CHINI

Country

Short Code

Kenya

22626

Uganda

7626

Nigeria

34350

South Africa

34624

Zambia

414

Malawi

15626

Sierraleone

2626

Zimbabwe

33334

Namibia

15626

Ghana

1474

Botswana

16626

Angola

44555

Ethiopia

8089

Rest Of Africa

(+)2783142100414

WAOKOENI WATANZANIA KWA KUWAPIGIA KURA BIG BROTHER

Mtanzania mwenzetu anaye tuwakilisha kwenye jumba la Big Brother katika shindani la 2013 Big Brother Africa 8 The Chase "Nando... [Read More]

 Wolper akiwa katika mazoezi ya viungo kujiweka teyari na mpambano wa kuzichapa na Mbunge wa Kawe Halima Mdee Julai 7 mwaka huu

WOLPER AJIKITA KWENYE MAZOEZI

 Wolper akiwa katika mazoezi ya viungo kujiweka teyari na mpambano wa kuzichapa na Mbunge wa Kawe Halima Mdee Julai 7 mwaka huu [Read More]


MSANII wa filamu nchini Jacqueline Wolper ameenda kujichimbia Afrika Kusini akifanya mazoezi ili ajiweke katika nafasi ya kuzichapa na mbunge wa CHADEMA Halima Mdee, katika tamasha la Matumaini litakalofanyika Julai 7 mwaka huu.

Wolper ambaye atapigana na Halima Mdee, alisema kuwa amejikita nchini humo kwa ajili ya kujiweka sawa ili aweze kumkabiri mbunge huyo.

Alisema mbali ya kujiweka fiti kwa ajili ya kumkabili mbunge huyo pia anajiweka fiti kwa ajili ya kujenga mwili wake ili kupunguza magonjwa pamoja na kujinginga na magonjwa ya kisukali yanayotokana na mafuta.

"Naamini nitamgaragaza mbunge huyo na sitochukua hata dakika tano kwenye mchezo huo kwani naamini mazoezi yangu ninayoyafanya ni njia moja wapo ya kujiweka vizuri kimwili" alisema Wolper.

Siku ya Usiku wa Matumaini utapambwa na mashindano kibao yakiwemo mbunge wa viti maalumu Ester Bulaya ambaye naye anatarajia kuzichapa na Aunt Ezekiel, huku Zitto Kabwe atazichapa na Vincent Kigosi

WOLPER KUZICHAPA NA HALIMA MDEE USIKU WA MATUMAINI

. MSANII wa filamu nchini Jacqueline Wolper ameenda kujichimbia Afrika Kusini akifanya mazoezi ili ajiweke katika nafasi ya kuzichapa na m... [Read More]


Kukanyaga bendera ya nchi yako ni wazi unaitusi nchi yako au ni kukosa heshima hayo ni maneno wanaojiuliza wamarekani walio wengi kutokana na kitendo alichokifanya mwanamuziki Lil Wayne kuikanyaga bendera ya nchi yake kwa makusudi kama vile tambala la deki.

Tukio hilo limetokea hivyo karibuni alipokuwa anafanya shoot muimbaji huyo alianza kurap mbele ya bendera kubwa ya Marekani ambayo baada ya muda ilitupwa chini na muimbaji huyo na kuikanyaga huku akiendelea kuimba.

Baada ya kushambuliwa na kushangazwa na mashabiki wake Lil Wayne ametoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo na kudai kuwa hakuikanyaga kwa maksudi kwani kipande kilichokuwepo kwenye nyimbo hilo kilionyesha kuimba kwa kutumia bendera hiyo lakini kuikanyaga ilikuwa ni bahati mbaya kwani hakuiona

LIL WAYNE APATA KASHIKASHI BAADA YA KUKANYAGA BENDERA YA MAREKANI

Kukanyaga bendera ya nchi yako ni wazi unaitusi nchi yako au ni kukosa heshima hayo ni maneno wanaojiuliza wamarekani walio wengi kutokan... [Read More]

Mwanamuziki wa nyimbo za kikabila Saida Karole hajapoteza maisha kama ilivyodaiwa katika habari za awali zilizopatikana kupitia mitandao mbalimbali,

Habari zilizothibitishwa na meneja wake ambaye yupo chini ya studio za Tivoli zimekanusha habari hiyo na kudai kuwa msanii huyo mzima na bado anaendelea na mambo yake

SAIDA KAROLI HAJAFA

Mwanamuziki wa nyimbo za kikabila Saida Karole hajapoteza maisha kama ilivyodaiwa katika habari za awali zilizopatikana kupitia mitandao m... [Read More]



 Jeneza lililobeba mwili wa msanii Langa likishushwa kwenye gari teyari kwa ajili ya kuupumzisha katika nyumba yake ya milele

 Msanii wa bongo fleva ambaye alikuwa swahiba wake wa karibu na msanii Ngwair M TO THE P pamoja na Mchizi Mox walihudhuria maziko ya msanii wa hip hop Langa Kileo yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
Baadhi ya ndugu, marafiki, na wasanii wakiupumzisha mwili wa Langa katika nyumba yake ya milele

MAZISHI YA LANGA KILEO YALIVYOFANYIKA KATIKA PICHA

 Jeneza lililobeba mwili wa msanii Langa likishushwa kwenye gari teyari kwa ajili ya kuupumzisha katika nyumba yake ya milele ... [Read More]


Waigizaji wa filamu nchini wanatarajia kugawa vyandarua kwa wagonjwa wa hospitali ya Seko Toure, wakati wa tamasha la Tanzania Open Film Festival (TOFF) linalotarajia kufanyika katika viwanja vya Sahara jijini Mwanza kuanzia Julai 1 hadi 7

Akizungumza jijini Dar es Salaam JB alisema kuwa kupitia jambo hilo wasanii wanapata fursa ya kukutana na moja kwa moja na mashabiki wao hivyo wamepanga kufanya kitu cha pekee

WASANII WA FILAMU KUGAWA VYANDARUA

Waigizaji wa filamu nchini wanatarajia kugawa vyandarua kwa wagonjwa wa hospitali ya Seko Toure, wakati wa tamasha la Tanzania Open Film ... [Read More]


Mwanamuziki Alicia Keys, amemzungumzia mke wa Rais wa Marekani Barak Obama , Michelle Obama kuwa ni mmoja wa wanawake wanaochangia kwa kiasi kikubwa kuwapa nguvu ya kufanya kile wanachokiamini kitawasaidia.

Keys alisema kuwa anakumbuka January mwaka huu walikuwa pamoja na mama huyo pamoja na mambo mengi alizungumza naye mambo mengi yanayohusu maisha hususani kwa wanawake ambao wanataka maendeleo kama yeye.

Alisema mfano mzuri kwake ni muimbaji mwenzake ambaye pia ni rafiki yake Rihanna anamuheshimu na kumpongeza kwa mafanikio yake ma kuwa ni mmoja ya wanawake wa kuigwa.

ALICIA KEYS AMPONGEZA MICHELLE OBAMA

Mwanamuziki Alicia Keys, amemzungumzia mke wa Rais wa Marekani Barak Obama , Michelle Obama kuwa ni mmoja wa wanawake wanaochangia kwa ki... [Read More]

LADY JD ATOA SHUKRANI KWA MASHABIKI WAKE

Mara baada ya kufanya vyema kwenye usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi,Lady Jd kwa mara ya kwanza amejitokeza na Kuzungumza na Pro-24 na k... [Read More]



MSANII wa filamu nchini Jacob Steven 'JB' aibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya msanii bora wa kiume huku Iren Paul kuibuka msanii bora wa kike katika tuzo kutoka kampuni ya Steps Entertainment zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Steps Entertainment ni kampuni ya usambazi wa filamu nchini ambapo kwa mara ya kwanza wameweza kuandaa tuzo hizo kwa ajili ya kutoa heshima na kutambua uwezo wa wasanii wa filamu pamoja na kuwapomgeza waliofanya vizuri.
Jb alitwaa tuzo hiyo kupitia movi inayojulikana kwa jina la Nakwenda kwa Mwanangu aliyocheza na msanii wa vichekesho King Majuto huku mzee huyo kuchukua tuzo ya mchekeshaji bora kwa kupitia movi hiyo.Katika kinyanga'nyiro hicho Jb aliweza kuwadondosha marehemu Steven Kanumba, Ray Kigosi, pamoja na msanii Cloud.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo alisema kuwa juhudi na kutambua unachotakiwa kufanya ni moja ya njia anayoitumia kumfikisha hapo alipo.Alisema kuwa kutokana na ubora alionao ni tuzo ya tatu anapokea kama msanii bora wa kiume hali hiyo inaonyesha anauwezo na jamii inapokea kazi zake na kuzitambua."
Hii ni tuzo ya tatu napokea kama msanii bora wa kike hali inayoonyesha kuwa nina uwezo na jamii nzima ambayo ndiyo mashabiki zangu wanatambua na wanaamini kazi zangu" alisema JB Wakati huo huyo filamu mwisho ya marehemu Steven Kanumba aliyoigiza na Jacqueline Wolper, inayojulikana kwa jina la Ndoa yangu imeibuka na tuzo ya kuwa ndiyo filamu iliyouza zaidi 'best selling movie'








MSANII wa filamu nchini Jacob Steven 'JB' aibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya msanii bora wa kiume huku Iren Paul kuibuka msanii bora wa kike katika tuzo kutoka kampuni ya Steps Entertainment zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Steps Entertainment ni kampuni ya usambazi wa filamu nchini ambapo kwa mara ya kwanza wameweza kuandaa tuzo hizo kwa ajili ya kutoa heshima na kutambua uwezo wa wasanii wa filamu pamoja na kuwapomgeza waliofanya vizuri.




Jb alitwaa tuzo hiyo kupitia movi inayojulikana kwa jina la Nakwenda kwa Mwanangu aliyocheza na msanii wa vichekesho King Majuto huku mzee huyo kuchukua tuzo ya mchekeshaji bora kwa kupitia movi hiyo.




Katika kinyanga'nyiro hicho Jb aliweza kuwadondosha marehemu Steven Kanumba, Ray Kigosi, pamoja na msanii Cloud.




Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo alisema kuwa juhudi na kutambua unachotakiwa kufanya ni moja ya njia anayoitumia kumfikisha hapo alipo.




Alisema kuwa kutokana na ubora alionao ni tuzo ya tatu anapokea kama msanii bora wa kiume hali hiyo inaonyesha anauwezo na jamii inapokea kazi zake na kuzitambua.




"Hii ni tuzo ya tatu napokea kama msanii bora wa kike hali inayoonyesha kuwa nina uwezo na jamii nzima ambayo ndiyo mashabiki zangu wanatambua na wanaamini kazi zangu" alisema JB




Wakati huo huyo filamu mwisho ya marehemu Steven Kanumba aliyoigiza na Jacqueline Wolper, inayojulikana kwa jina la Ndoa yangu imeibuka na tuzo ya kuwa ndiyo filamu iliyouza zaidi 'best selling movie'

JB ATWAA TUZO YA MSANII BORA WA FILAMU, FILAMU YA NDOA YANGU YAIBUKA KIDEDEA KWENYE MAUZO

MSANII wa filamu nchini Jacob Steven 'JB' aibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya msanii bora wa kiume huku Iren Paul kuibuka msa... [Read More]


HATIMAYE  Kanye West aitwa baba baada ya mpenzi wake Kimberly Noel 'Kim Kardashian' kujifungua mtoto wa kike mwishoni  mwa wiki.

Kim Kardashian alijifungua siku ya Jumamosi katika hospitali ya Cedars- Sinai Medical Center jijini Los Angeles kabla ya siku iliyokuwa inatarajiwa, huku tarehe halisi ya kujifungua ilitazamiwa kuwa Julai 11

Vyanzo vya habari vya karibu na mwanadada huyo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Kim alijifungua salama kwa njia ya kawaida huku akiwa amewahi tarehe yake iliyotizamwa kujifungua.

Vyanzo hivyo viliendelea kuubanisha mtandao huo kuwa kutokana na hali ya Kim kuwa mbaya Kanye alilazimika kutohudhuria shoo yake iiliyokuwa inajulikana kwa jina la 'listening part' ya albamu yake mpya siku iliyofuata aliweza kuongozana na mpenzi wake hospitali.

Wote wawili wakiwa ndio mara ya kwanza kupata mtoto, historia inaonyesha kuwa walikuwa wapenzi tangu Aprili 2012.

KIMM KARDASHIAN APATA MTOTO WA KIKE

HATIMAYE  Kanye West aitwa baba baada ya mpenzi wake Kimberly Noel 'Kim Kardashian' kujifungua mtoto wa kike mwishoni  mwa wiki. ... [Read More]

Yafuatayo ni majina ya washindi wa tuzo za filamu kwa mwaka 2012/13 toka kampuni ya steps entertainment zilizofanyika juzi usiku kwenye ukumbi wa hoteli ya blue Pearl iliyopo ubungo jijini Dar es Salaam.

Katika tuzo hizi Merehemu steven Kanumba aling’ara kwa kupata tuzo nyingi kuliko waigizaji wote kwa kupata tuzo tatu.

Mwigizaji bora wa kiume ni JB kupitia filamu ya ‘Nakwenda kwa mwanangu’ aliyocheza na mzee Majuto.

1.Best Director : Ray Kigozi (Women Of Principle)

2.Best Actor: Jacob Steven ( Nakwenda Kwa Mwanangu )

3.Best Actress : Iree Paul

4.Best Movie : – Kijiji Cha Tambua Haki

5.Best Selling Movie :- Ndoa Yangu

6..Best Best Story :- Nice Muhammed (Baamed)

7.Best Screen Play :- Ally Yakuti

8.Best Cameraman :- Zakayo Magulu

9.Best Sound :- Bharghasi Saidi

10.Best Editor : Timoth Conrady

11.Best Production House:RJ Production Company

12.Best Supporting Actor : Rado (I think I hate my wife )

13.Best Supporting Actress: Riama Ally ( Tabu Ya kuolewana)

14.Best Producer : John Lister

15.Best Comedian :King Majuto

16.Most Promising Actor : Niva

17.Most Promising Actress : Irene Paul

18.Best Child Artist : Jennifer

19.Best Action Movie ouble J

20.Best Perfomance in a negative role : Mohammed Nurdin -checkbudi (Azma)

21.Special Jury Award : Jennifer Kyaka (odama)

21.Best movie on National Integration:Mwalimu Nyerere

22.Best Movie for the development of culture & Language :Toba

23.Posthumous Awards :- Late:Kanumba, Late:Sajuki , Late:Sharobaro,Late:Johna

MAJINA YA WASHINDI WA TUZO ZA FILAMU ZA STEPS ENTERTAINMENT HAYA HAPA

Yafuatayo ni majina ya washindi wa tuzo za filamu kwa mwaka 2012/13 toka kampuni ya steps entertainment zilizofanyika juzi usiku kwenye ... [Read More]

TANK FEAT. CHRIS BROWN - SHOTS FIRED

[Read More]

 Huyu naye alikuwepo ili kuonyesha uhalisia wa jina la Anaconda ambalo sasa anatumia msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Jay Dee, ambapo jina hilo limetokana na vuguvugu ambalo linaendelea hivi sasa ambalo hilo vuguvugu ndilo limechangia shoo ya mwanamuziki huyo kujaa huku mashabiki wakionyesha hali ya kumshinda mtu anyemkandamiza msanii huyo

CHIMBUKO LA JINA LA ANACONDA ANALOTUMIA JAYDEE

 Huyu naye alikuwepo ili kuonyesha uhalisia wa jina la Anaconda ambalo sasa anatumia msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Jay D... [Read More]

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging